Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, July 6, 2013

JOYCE KIRIA AELEZEA SAFARI YAKE YA TABORA KUMWONA MUME WAKE ILIVYOKUWA


Safari yangu kuelekea mkoani tabora ilikuwa na changamoto nyingi, Ila kubwa namshukuru Mungu nilifika salama na kurudi salama. Najua kuna FANS wangu wengi wananipa support haswa katika maombi ya familia yangu. So najua itakuwa vizuri kama nitashare na nyie jinsi safari yangu nzima ilivyokuwa.
Nimetumia siku tano so nitakuwa naielezea kwa day after day ila briefly ili iwe rahisi kujua yote toka naenda mpaka narudi.



Ila wakati naipanga hii safari ili kwenda kumuona mume wangu, iliniweka katika wakati na maamuzi magumu sana kama fans zangu mnavyofahamu nina watoto wadogo akiwepo mdogo wa miezi mine 4,  Tabora ni mbali sana ni mwendo wa karibia masaa 14 kutokea Dar Es Salaam watoto ni wadogo nikisafiri nao nikaona nitakuwa nawatesa,  Nikafanya maamuzi magumu mno ya kuwaacha wanangu kwa wadada wasaidizi wangu wa nyumbani. Hizi ni changamoto za maisha inapofika wakati mgumu kama huu ulionifikia mimi inabidi ufanye maamuzi mazito, so nikawaacha wanagu Lincon na Linstone.
Lincon na Mdogo Wake Linston.
                           DAY1. IJUMAA 28/06/2013
Siku ya Ijumaa tarehe 28/June Tulikutana Ubungo, Tukitumia usafiri binafsi na tulikuwa watu 5. Tukaanza safari yetu na tunamshukuru Mungu tulifika salama Mkoani Morogoro, Tukaendelea na safari  Ila tukiwa kati ya Morogoro na Dodoma gari yetu kidogo ikaleta tabu,
 hapa ni kati ya Moro na Dom
Baridi ya hapa ilikuwa ni balaa.
hapa baba mkwe akicheki tatizo la gari.
Baada ya dk kadhaa gari ikawa iko poa.
 Baada ya gari kuwa poa tukaendelea kwa safari tukaingia Dodoma, Tukapata chai kidogo 
Tukisubiria Chai hapa ni Dodoma.
 Baada ya chai tukirudi garini kuendelea na safari.
 na gari nayo ikapata lishe/mafuta.
then tukaendelea na safari. 
Tulipofika Ikungi  Kabla hatujafika Singida mjini gari ikaharibika tena , dereva akasema ni tatizo dogo linarekebishika fasta then tutaendelea na safari.
 Tukapata Fundi pale pale Ikungi, hapa akitazama tatizo.
dah ikawa vise versa tatizo likawa kubwa, it was around saa tisa hivi alasiri tupo Ikungi, mpaka saa 6 usiku gari haikufaa ikabidi tutafute hotel kulala hapo.
 Mida ya saa sita hivi gari ikawa bado haijatengamaa.

                                  DAY2.JUMAMOSI 29/06/2013
Siku ya pili tukaamka na kujiandaa, ila mpaka tunamalizia kujiandaa gari ilikuwa bado haijatengamaa, ili wote tusiwe tumestuck sehemu moja tukaamua kugawana wengine wabaki na gari na wengine tutangulie. Kutokea hapo Ikungi tukapata usafiri wa NOAH mpaka Singida Mjini si Mbali sana ilikuwa mwendo kama wa dk 20 ama 30 hivi, Tulipofika Singida Mjini tukapata HIACE ambayo tulianza safari kuelekea Igunga.
 hapa ilibidi tufanye safari za kuunga unga mana usafiri pia ulikuwa wa tabu, 
mwendo wa masaa kama mawili na nusu ama matatu tukawa tumefika Igunga, tukakata tiketi za kuelekea Tabora mjini..
 Hapa ni stendi Igunga tukisubiria basi,huyu ni dereva wa Hiace Tuliyokuwa tumepanda.
 Usafiri ni wa Tabu mno tukapata basi ila tulikosa siti takasimama ,
 it was a very rough road kutokea hapo Igunga mpaka Tabora mjini na ni mwendo karibu wa masaa 3 na nusu hivi, Ila Mungu alisadia tukafika salama Tabora mjini mida ya saa 11 kama na dk 20
 Mwenyeji wetu akitusaidia kutuonyesha hoteli.
Kutoka stendi ya mabasi mpaka ilipo hoteli ni mwendo wa dk 2 tu kwa miguu.
na kuanza tafuta hotel. By the way nilitamani sana nikiingia Tabora nielekee Gerezani Ila nilikuwa nilishachelewa kwa kuuuliza uliza niliambiwa Kutembelea gerezani mwisho ni saa 9 alasiri.
 Uchovu wa safari.
Katika kuulizia ulizia hoteli tukapelekwa Hotel inaitwa Mwafrika Hotel, Pale Tulikosa nafasi ila meneja wa pale akachukua jukumu la kututafutia sehemu nyingine , tukapata sehemu nyingine lakini tukapanga next day wakitoka watu tutarudi pale.
 Aliyevaa Jezi ni Meneja Wa Mwafrika Hoteli, Anayenielekeza ni Mmiliki wa Mwafrika Hotel.
Huyu ni shemeji yangu kabisa kabisa, ni mume wa dada yangu"post ya changamoto na Opportunity" mtamfahamu vyema. Hapa ndo alituchukua na kutupeleka hotel nyingine kwa usiku huu.

                                        DAY3. JUMAPILI
Tuliamka asubuhi tukajiandaa kuelekea gereza Kuu Uyui, ila tulipitia Mwafrika hotel kuacha mizigo yetu mana kwa siku hiyo tutakuwa pale.
Then safari ya kuelekea Gereza Kuu la Uyui,
 Si mabali kutokea pale Tabora Mjini ni kama mwendo wa Dk 5 hivi kwa Gari, tukawa tumefika gerezani pale, Tukaelekezwa taratibu za kufuata kujiandikisha na kila kitu halafu tukaambiwa tusubiri kwa zamu yetu mana pia tulikuta watu wengine ambao nao walikuwepo pale kuwaona ndugu jamaa na marafiki zao. Muda wetu ulipofika na sie tukaitwa katika listi tukapelekwa huko gerezani, hapo mapokezi kuna sheria zao za kuzima simu na kuacha kila kitu so baada ya kuacha tukaingia katika hiko kijichumba kidogo tu.
Kiukweli it was a very SAD moment, nilipomuona mume wangu, akiwa kwa upande wa pili na sikuwa namuona vizuri mana hiyo nyavu iliyotenganisha hapo ilikuwa kuu kuu, Nilishindwa Kujizui MACHOZI yalianza kunitoka, Ila mume wangu alikuwa MORE THAN STRONG akinisihi nisilie ye yuko poa, Kiukweli Kauli hii ilinipa nguvu, nikashangaa na mie Napata nguvu. Swali la Kwanza aliniuliza Vipi WATOTO hawajambo? Umekuja Nao? Nikamjibu wako salama , Kutokana na umbali wa safari nimeonelea nisije nao”Hapa Pia Naendelea Kuamini Kuwa MUNGU bado Yuko Upande Wetu, Misukosuko niliyoipata njiani nawaza ningekuwa na watoto ingekuwaje”?? .Tukaongea mawili matatu kama dakika tano hivi tukaambiwa muda umekwisha tunatakiwa kutoka. Kuna nguo nilibeba tukaambiwa zikakaguliwe kwanza then ndo atakabidhiwa tukafanya kama maelezo yalivyotaka then tukaondoka.
Kiukweli after  kumuona mume wangu hapo ndo nikawa na uhakika wa aslimia mia kuwa yuko mahali Fulani nikarudi zangu hoteli, ila nilipata mda mchache sana na nilikuwa na maswali kibao, tukaulizia taratibu za pale wakatuambia kwa waliotoka mbali huwa wanapata nafasi siku za kazi kwa at least hata dk kumi, so nikipanga kurudi tena siku ya Jumatatu.
 Jioni Baada ya Kutoka Gerezani, Nilikutana na Sister Wangu ambaye hatujaonana zaidi ya miaka 20. Kwenye post ya changamoto na opportunity nae mtamfahamu.
                                            DAY4.JUMATATU
Niliamka asubuhi na kujiandaa, Baada ya kumaliza nikatoka kwenda kutafuta baadhi ya vitu alivyoniagiza, So nilipokamilisha vyote nikaanza safari ya kwenda Gereza Kuu Uyui kwa siku nyingine tena, Leo nikiwa nimeongozana na mwanasheria  ambaye yeye anafanya shughuli zake kule kule kwa ajili ya mambo mawili matatu. 
Tukafuata taratibu zao kama kawaida kuandikisha, na baada ya muda tukapata nafasi  ya kwenda kumuona, Leo Kidogo ikawa  nafuu kwa vile tunatoka mbali” ipo sheria kabisa kwa mtu mfano anayetoka mbali na Tabora kuwepa nafasi kidogo zaidi mana ametokea mbali “. Kama Kawaida ya pale tukatakiwa kuacha kila kitu na siimu kuzizima, tulichoruhusiwa kupita nacho leo hii ilikuwa ni pesa tu,
 Nikiwa na mwanasheria.
Tukapelekwa katika chumba cha wazi ni pa kuonea wafunga tulikuwa  chini ya ulinzi mkali wa uangalizi wa askari si chini ya 7, akiwepo askari mmoja wa kike , na masharti makubwa mawili hakuna kulia na hakuna kuongea kwa kunong’ona “WHISPER”. Dah kweli ilikuwa ni wakati mgumu hali ambayo nilikuwa naisikia uchungu then napewa masharti hakuna kulia, Ila narudia kusema Mungu hawezi Kuniacha , Nilipata Ujasiri wa ajabu na kuacha kulia na kuanza kuongea mawili matatu kuhusu familia na kuhusu maswala ya kazi, Ila pia napo kama after dakika kumi tukaambiwa muda umekwisha tunatakiwa kutoka . Tukatoka na kurudi zetu hotelini. Usafiri wa Tabora kwa sasa ni tabu tukakosa usafiri wa kurudi Dar kwa siku ya Jumanne.
 Hapa Nikiagana na Mwanasheria.

                                                     DAY5.JUMANNE
Baada ya kukosa usafiri wa kurudi Dar Siku ya Jumanne, nikitazama Tabora ni mbali nikasema ngoja niende Gerezani kuomba hata dakika moja ya kumuaga mume wangu, nikaelekea gerezani Uyui, Ila dah nikaomba sana wanilikatalia, nikaamua kurudi zangu kiunyonge hotelini, kuja kusubiria Jumatano kusafiri kurudi zangu Dar.
                                              DAY6.JUMATANO
Nikaanza safari ya kurudi dar, Tuliondoka Tabora saa 12 asubuhi, After Masaa Mengi njiani by saa 2 na nusu hivi nikafika salama Dar, nilikuwa So excited kuwaona wanangu, Thanx God Nilifika salama na niliwakuta wanangu wako salama.
NYONGEZA
Jumatatu tarehe 8/Julai/2013, mume wangu anapandishwa tena mahakamani huko Tabora, Bado nahitaji msaada wenu katika kunisaidia maombi.

No comments:

Post a Comment