Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akiteremka kwenye ndege GF1 alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam akitokea Nchini Nigeria
alikohudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika uliojadili mbinu za kukabiliana
na Ukimwi, Malaria na kifua kikuu ambapo aliwaambia wajumbe wa mkutano
huo kuwa Tanzania itafikia malengo ya Umoja wa Afrika iliyojiwekea
katika kukabiliana na Magonjwa hayo, mkutano huo ulimalizika jana July
17-2013 mjini Abuja Nchini Nigeria (Picha na OMR) Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal
akipokelewa na baadhi ya viongozi wa serikali baada ya kuwasili uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Msafara wa Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib
ukiondoka uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini
Dar es salaam . Makamu wa Rais ametokea nchini Nigeria alikohudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika uliojadili mbinu za kukabiliana na Ukimwi, Malaria na kifua kikuu
ISSA GAVU ATOA ZAWADI KWA WASHINDI WA MASHINDANO YA MICHEZO MBALIMBALI -
UNGUJA
-
Mwakilishi wa Jimbo la Chwaka Mkoa kusini Unguja Mhe. Issa Ussi Gavu ambaye
ni Katibu wa Oganazesheni wa CCM Taifa (MCC) ametoa zawadi mbalimbali za
medali...
2 hours ago
No comments:
Post a Comment