Na Mwandishi Wetu
HOSTI wa Kipindi cha ‘The Mboni Show‘ kinachorushwa kupitia Kituo cha
Runinga cha EATV, Mboni Masimba Jumapili iliyopita aliangua kilio mbele
ya Rais Mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi walipokuwa kwenye hafla
ya kufuturisha kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_s1AUgBitzEg4q3KnHMZUeQH_8eLhvvHRLJBzwiT937Z1XGjshZtt5pp6MOABmPBmR2Z7ggatdrwoB3FcAmx2iEW5ughaaRSkwezlnkagLx93hc5IlcYLQdcP15-kdlRUPEPxcRrOjNMHG6npMU1YvLbNi0IaBQJp4yiO38oEFouAytH9iN1ABW8p81c4PCi1vsUHm1iQn0go33u67be6pSaHk8RQWIFqqX7rzDMniRag1r=s0-d)
Mtangazaji
huyo alimwaga machozi wakati akiwakaribisha wageni waalikwa pamoja na
kutoa shukrani zake kwa wote waliomsaidia kufanikisha shughuli hiyo.
Baada ya kutoa shukrani alionekana kuwa mwenye furaha kwa kumtambulisha
baba yake mzazi, mzee Masimba ambaye hajulikani kwa watu kama ilivyo
kwa mama yake.
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_s60cJvCWqCE70jYFqxkpE8hHvtAO8zGtlxuMbntlDCA931Xf9R1DQWGRt7JfMuExv5Er016zSflRuDpWcMHlurBqv4bwF5qtPw1WOWg3B6E_85pCTn-faUhZ2urKFSttRT4u-WkPiNYsAeJfsqMmqt7-lQWkhEqb80-FqxPpdiSRudQyTOwmlAnG6bADtSm_Oh3V-rZBbuCI28gnwQfv_GPk1EliyrBOo829LdPtVeifP6=s0-d)
Aidha,
mtangazaji huyo alimwita mama yake, bila ya kutarajiwa akaanza kumuomba
msamaha mzazi wake huyo kwa kumsumbua na kumuahidi kwamba
amejirekebisha.
“Nakuomba msamaha mama yangu, Mboni si yule tena
nimebadilika, nisamehe sana,“ alisema Mboni kisha akaangua kilio kujutia
makosa yake.
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_tujmDTRFJvZ_J--vsc2pHCGNfkDcNseFshuooQFiyPM6E-SHeuc3oGGYjuTAWcVL2IQEIZV3Op5Bc7vKdq3UNLF3JC4rRU6jxtfo88T4mypMbfzW7kVE06vqKx3bp1atGjsuB2LBvrop-3BPrESSOdcWMMoRcTL2_Z0oQLSSM0EZ3bfkSDk9k0ZuJhmOT1AFWuxlv6QLWlzoSFa8m-9X6fnUXuFUkTKN57v66CZHUnD129vN4s5lpq=s0-d)
Baada
ya tukio hilo, Mboni alisikika akiomba dua kwa Mwenyezi Mungu ili ampe
mume mwema. Mtangazaji huyo alirudia mara kwa mara kipengele hicho cha
kuomba mume kiasi cha baadhi ya wageni waalikwa kusema kwamba ni kweli
anahitaji mume kwani umri wake unahitaji kuwa na familia.
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_vVFvrqYeMB03hOV2vgZUu_c-jv-q2anieV3FCF7dcKvHRTpFm-TEsSTpEBlcs0jniJsZkDT8SmyujWti_nY4pPuwa9J6axL7i7k8emrQd0-5q1oXdx0BHt_wGN7k8xXyyJCoYIyQCEImy4CQ_PQT1SHJme326b7KdOR-wCpJzV1KxkBCVoppNZxTtgBv_8h8SQbPQJVvfJ_NMhV9kVjThTV3HUR7Wiha4rcW7rA26pgk1G=s0-d)
Mbali
na matukio hayo, Mboni alitambulisha vituo viwili vya watoto yatima
ambavyo anavihudumia kupitia kampuni yake ya The Mboni. Mbali na Mwinyi
wageni wengine walikuwa ni Shehe wa Mko wa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa
Salum, Asha Rose Migiro pamoja na Khadija Mwanamboka.
Wengine ni Shay-rose Bhanji na baadhi ya wanamuziki wa The Kilimanjaro ‘Wana Njenje’ Steve Nyerere na watu wengine maarufu.
Habari imeandikwa na Hamida Hassan, Imelda Mtema, Musa Mateja na Shakoor Jongo.
No comments:
Post a Comment