Pages

Sunday, July 21, 2013

MTAFARUKU WA VIMINI HOSPITALI TEULE DODOMA


Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma Dk. Ezekiel Mpuya amesema tangazo lililotolewa hospitalini hapo la kuwataka watu kuvaa mavazi ya heshima wanapoingia hospitalini hapo lilikuwa likihusu watumishi wa hospitali hiyo na si wananchi wa kawaida.
Akizungumzia suala hilo jana, Dk Mpuya alisema kuwa Katibu wa Hospitali hiyo alitoa tangazo hilo kimakosa hali ambayo ilisababisha walinzi kuzuia watu waliovaa ‘ovyo’ kuingia hospitalini hapo.

“Uongozi wa hospitali unaomba radhi kwa usumbufu waliopata wagonjwa na wananchi waliofika hospitalini hapo kwani tangazo lilitolewa kimakosa na katibu kwani lilikuwa likiwahusu watumishi pekee na si wananchi” alisema Dk. Mpuya

No comments:

Post a Comment