Mwenge
huo wa Uhuru umetembelea miradi 23 ya maendeleo na miradi 28 ya vikundi
Mkoani Rukwa vyenye thamani ya fedha za kitanzania zaidi ya shilingi
bilioni 3.4 ikiwa ni mchango wa Serikali kuu, Halmashauri, Wananchi na
Wadau wengine wa maendeleo.
Ndege
ndogo ya Shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) ikipaa angani katika
uwanja wa ndege wa Sumbawanga leo tarehe 23 Julai 2013 ikiwa na Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya, wakimbiza Mwenge wa Uhuru
kitaifa sita pamoja na Mwenge wa Uhuru utakaoenda kukabidhiwa Mkoani
Tabora na Mkuu huyo wa Mkoa wa Rukwa. Wakimbiza mwenge hao ni Ndugu Juma
Ali Simai (Kiongozi), Zamda A. John, Christopher Emmanuel, Seperatus
Lubinga, Zuwena Abdallah na Mgeni S. Mgeni.
Mkuu
wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Mhandisi Stella Manyanya Mwenge wa Uhuru mara baada ya kukamilisha
ratiba yake katika Wilaya hiyo na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla. Mkuu huyo
wa Mkoa atasafiri kwa ndege kuukabidhi Mwenge huo Mkoani Tabora.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akitoa hotuba ya kuwaaga
wakimbiza mwenge kitaifa na Mwenge wa Uhuru muda mfupi kabla ya kusafiri
na Mwenge huo kwa ajili ya kuukabidhi Mkoani Tabora mapema leo tarehe
23 Julai 2013. Katika hotuba yake hiyo aliwapongeza wakimbiza Mwenge
wote na wananchi Mkoani Rukwa kwa kufanikisha zoezi hilo kikamilifu na
kuwapa vyeti vya pongezi wakimbiza Mwenge hao wa kitaifa.
Picha
ya pamoja kati ya kikundi cha matarumbeta kilichokuwa mstari wa mbele
katika kutumbuiza kwenye ziara ya Mwenge Mkoani Rukwa na baadhi ya
wakimbiza Mwenge kitaifa na mratibu wa Mwenge Mkoa wa Rukwa Ndugu
Abubakari Serungwe wa kwanza kulia (mbele).
Kiongozi
wa mbio za mwenge kitaifa Ndugu Juma Ali Simai akizungumza na wananchi
wa Manispaa ya Sumbawanga katika Stendi kuu ya mabasi Mjini Sumbawanga
tarehe 22 Julai 2013. Kulia ni Diwani wa kata ya katandala Ndugu
Kisabwite na Mbunge Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal.
Mkuu
wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kmanta akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya
Kalambo Moshi Chang’a Mwenge wa Uhuru mara baada ya kumaliza mbio zake
Wilayani humo tarehe 20 Julai 2013.
Mkuu
wa Wilaya ya Kalambo machachari katika mbio za mwenge wa Uhuru Moshi
Chang’a akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka Mwenge
wa Uhuru mara baada ya kumaliza mbio zake Wilayani Kalambo tarehe 21
Julai 2013
Mkuu
wa Wilaya ya Sumbawanga Methwew Sedoyyeka akipokea mwenge wa Uhuru
kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang’a tarehe 21 Julai 2013
na kuahidi kuukimbiza katika wilaya yake kwa amani, nguvu na uadilifu
mkubwa.
Baadhi ya raia wa kigeni nao waliomba kupiga picha na Mwenge wetu wa Uhuru.
Wananchi
na wanafunzi walihamasika vya kutosha na Mwenge wa Uhuru kiasi cha
wengine kupanda juu ya miti ili waweze kupata taswira yake mwanana.
Wanafunzi na wananchi wakiwa juu ya miti kushuhudia Mwenge wa Uhuru na ujumbe wake.
Kwa wengine kuuona Mwenge wa Uhuru vizuri haikuwa kazi rahisi walilazimika hata kuhatarisha maisha yao.
Picha
ya pamoja kati ya mratibu wa Mwenge Mkoani Rukwa ndugu Abubakar
Serungwe na baadhi ya wakimbiza mwenge kitaifa pamoja na katibu wa CCM
Sumbawanga Mjini Mama Silaf Maufi.
(Picha na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa “rukwareview.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment