The
Cranes itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa
5.30 asubuhi kwa ndege ya Air Uganda ambapo itafikia hoteli ya Sapphire
iliyoko maeneo ya Kariakoo.
Waamuzi
wa mechi hiyo ambao wanatoka Burundi nao watawasili kesho saa 9.35 kwa
ndege ya Kenya Airways. Naye Kamishna wa mechi hiyo Tesfaye Gebreyesus
kutoka Eritrea atatua nchini keshokutwa alfajiri kwa ndege ya EgyptAir.
Maofisa
wote hao wa mechi hiyo watafikia hoteli ya New Africa. Mkutano wa
maandalizi ya mechi utafanyika Ijumaa saa 10 jioni Uwanja wa Taifa, na
utakuwa chini ya Gebreyesus.
No comments:
Post a Comment