Pages

Thursday, July 25, 2013

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MLOWA WANUSURIKA KIFO MARA BAADA YA BWENI KUSHIKA MOTO HUKO IRINGA


 WANAFUNZI 12 wa Shule ya Sekondari ya Mlowa iliyopo Wilaya ya Iringa Vijijini wamenusurika kufa baada ya bweni walilokuwa wamelala kuungua kwa moto na kuteketeza vitu ambayo vilikuwemo ndani. Tukio hilo linadaiwa lilitokea baada ya hitilafu ya umeme wa nishati ya jua (Sola) iliyosababishwa na wanafunzi ambao walikuwa wamelala katika bweni hilo kuunganisha nyaya kienyeji kwa ajili ya kusikiliza redio na kusababisha hasara ambayo inakadiriwa kufikia sh. milioni 1.8.

Akizungumzia jana ofisini kwake juu ya tukio hilo la kuungua kwa bweni na kunusurika kwa wanafunzi, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mlowa, Mwalimu Frank Mahai alisema wanafunzi wa l i o n u s u r i k a awa l i walikuwa wanaishi nje ya shule.Alisema, mipango ya kuishi katika bweni hilo ilifanywa katika kikao cha wazazi na walimu kwa ajili ya wanafunzi ambao wanatoka mbali na shule ili wapate mahali pa kuishi katika muhula wa mitihani ya mwisho.
Mkuu huyo alisema kuwa, wanafunzi wengine wa shule hiyo wakati inaungua walikuwa wamekwenda kucheza mpira wa miguu kwa wavulana na wasichana katika Shule ya Sekondari ya Kalenga na kubakia wanafunzi 12 katika bweni ambapo saa 1:30 jioni moto ulianza kuunguza bweni hilo.

“Wanafunzi waliohusika na kuunguza ni baada ya kuunganisha nyaya kienyeji na kusababisha shoti hadi kuunguza bweni hilo,” alisema Mkuu huyo. Alivitaja vitu vilivyoungua kuwa ni pamoja na nguo za wanafunzi, mabegi, madaftari, magodoro pamoja na paneli za sola ambazo zimeteketea moja kwa moja pamoja na dari ya chumba cha bweni ambapo jumla ya gharama zake zinafikia kiasi hicho cha fedha.

Hata hivyo Diwani wa Kata ya Mlowa, Charles Nyagawa (CCM) akizungumzia tukio hilo alisema kuwa amesikitishwa na kuungua kwa bweni hilo ambalo wazazi walishiriki kujenga na walitumia gharama kubwa.

Diwani huyo alisema, amesikitishwa na tabia za wanafunzi kuunguza bweni hilo kutokana na kujiingiza kwenye ufundi ambao hawaujui na wala hawana utaalamu nao.
Al i s ema k uwa , p i a anawashukuru wazazi na wananchi ambao walifika katika kijiji hicho na kuuzima moto na kuwa i n g awa h awa k uwe z a kufanikiwa anawashukuru kwa ushirikiano ambao w a l i u o n e s h a k a t i k a kuhakikisha moto huo unazimika na kuokoa baadhi ya mabweni mengine yasiendelee kuungua moto na kuteketea mali zingine zikiwemo za wanafunzi ambao walikwenda kwenye michezo na vitabu vya shule

No comments:

Post a Comment