Pages

Thursday, July 4, 2013

WAPENZI WAWILI WATOLEWA TAIRI ZA GARI LAO BAADA YA KUEGESHA KWENYA NYUMBA YA MTU BILA TAARIFA USIKU NA KISHA KULALA.





 Kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Njombe Mjini Bwana Donald Mng'ong'o Katikati ni Mwenyekiti wa Mtaa Kambarage Bwana Pancras Matinya na Kulia ni Afisa Mtendaji wa Mtaa Huo Bi.Telesina Manga wakitolea Maelezo hayo mara baada ya Maaafisa wa 
Polisi Kufika katika Eneo Hilo leo Kushuhudia Tukio Hilo.
 Wapenzi waliosababisha Hofu kubwa kwa Wakazi wa Kambarage Mjini Njombe baada ya Kupaki Gari lao Kwenye Nyumba ya Mtu walipo Lewa Pombe na Kisha Kulala kwenye Binti Huyo hali iliyopelekea Serikali ya Mtaa Kulazimika Kufungua Tairi za Nyuma Ili kumpata Mhusika ambaye amejitokeza Asubuhi ya Leo.


 Binti aliyevalia Kofia ya CHADEMA Ndiye aliye Lala na Jamaa Huyo Chumbani Kwake hadi hali hiyo Kujitokeza.
 Benedict akitoa Namba yake kwa Askari Polisi kwa Mawasiliano baada ya Kukamilisha Taratibu za Ofisi ya Mtaa wa Kambarage Mjini Njombe.
 Chumba cha Kwanza ndiko Jamaa Huyo alipo Lala na Mpenzi wake baada ya Kufanya Maegesho kya Gari Lake Kwenye Nyumba ya Jirani yake Usiku Mzima na Kisha Wananchi Kutoa Matairi.
 Binti wa Mtuhumiwa aliyepaki gari kwenye Nyumba ya Bwana Lupenza Kambarage Bi.Lamar ambaye ni Mpenzi Wake akielekea Nyumbani Waliko Lala wakati Wananchi wakihangaika Usiku Mzima na Serikali Kumtafuta Mwenye Gari Hilo.


Katika Hali Isiyo ya Kawaida Wananchi wa Mtaa wa Kambarage wamejikuta Wakiingiwa na Hofu Kubwa kutokana na Mtu Mmoja anaye Fahamika kwa Jina la Ben Matimbwi Mkazi wa Njombe kuegesha Gari Lake Kwenye Nyumba ya Bwana Lupenza Usiku wa Kuamkia Leo Bila Taarifa na Kisha kwenda Kulala kwa Mpenzi wake.
Kutokana na Matukio ya Mara kwa Mara yanayojitokeza katika Mtaa Huo Wananchi Hao Pamoja na Uongozi wa Serikali Ya Mtaa Huo walilazimika Kufungua Matairi ya NYUMA ya Gari Hilo baada ya Mwenye Gari kutopatikana Wakidhani Huenda Gari Hilo hutumika kwenye Matukio.
Pancras Matinya ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Kambarage ambaye amesema Licha ya wao Kuripoti Polisi kutokana na Tukio Hilo lakini Mmiliki wa Gari Hilo anatakiwa Kulipa Faini ya USUMBUFU Kwa Wakazi wa eneo Hilo na Uongozi Serikali kwani Usiku huo wamepata Shida ya Kumtafuta Bwana Matimbwi Bila Mafanikio akiwa Amelala na Mpenzi Wake.
Mtandao huu wa www.gabrielkilamlya.blogspot.com ulizungumza na Binti Huyo anayefahamika kwa Jina la Lamar Nuru ambaye amesema kuwa Tatizo Lililopelekea kujitokeza kwa Tatizo hilo ni Kutokana na Mpenzi wake bwana Matimbwi kunywa Pombe na Kulewa kisha Kuegesha Gari lake kwenye Nyumba ya Mtu Jirani na walipo lala.
Kwa Upande wake Bwana Benedict Matimbwi ambaye ni Mmiliki wa Gari Hilo amekiri kuwa Alikwenda Kunywa Pombe katika Mtaa Huo mara Baada ya Kulewa sana Alishindwa Kurudi Nyumbani Kwake na Kisha Kulazimika Kulala na Mpenzi Wake Huyo.
Bwana Matimbwi Ameongeza Kuwa Asubuhi wakati Akiamka kwa Mpenzi wake ndipo alipo kuta Gari lake limetolewa Tairi zote za nyuma ndipo alipo lazimika kuanza Kuulizia na kupata taarifa hizo na kisha kuwasiliana na Ofisi ya Serikali ambao akaambiwa asubiri Jeshi la Polisi lifike kwani wameshatoa taarifa Huko.

No comments:

Post a Comment