Wanawake na akina dada wanaopenda ngozi zao kuwa nyororo, kuondoa mikunjo na uchafu hutembelea katika saluni ya Ci:z.Labo ambayo hutoa huduma hiyo ya kutengeneza ngozi kwa kutumia konokono 'Snail Facial '.
Mmoja wa wafanyakazi katika saluni hiyo, Manami Takamura anaeleza kuwa uterezi anaouacha konokono katika ngozi huondoa seli za zamani, hutibu ngozi baada ya kuunguzwa na jua pamoja na kuilainisha.
Huduma hiyo kwa saa moja inagharimu kiasi cha pauni 161 ambazo ni sawa na shilingi 392,951 za Kitanzania. Kwa kiasi hicho mteja uanza kwa kuoshwa kabla ya konokono hao kupitishwa katika uso wake. Baadaye hufuata huduma nyinginezo zianazoambatana na utengenezaji wa ngozi.
Baadhi ya wateja waliopata huduma katika saluni hiyo wanasifia huduma hiyo na kuwa imefanya ngozi zao ziwe nyororo na za kuvutia.
No comments:
Post a Comment