Abiria wawili wamefariki dunia na wengine 63 wamejeruhiwa na kulazwa
katika vituo vya afya kadhaa, zahanati pamoja na Hospitali Teule ya
Rufaa ya Mkoa wa Pwani baada ya basi mali ya Kampuni ya Meridian kuacha
njia na kupinduka jana katika Barabara Kuu ya Chalinze- Segera wilayani
Bagamoyo mkoani Pwani.
Abiria
waliofariki ni miongoni mwa majeruhi 24 wa ajali hiyo ambao walipelekwa
moja kwa moja kupata matibabu katika Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa
Pwani, Tumbi baada ya hali zao kuonekana ni mbaya zaidi ya wengine
katika eneo la tukio. Wengi walikuwa wamevunjika sehemu mbalimbali za
miili yao.
Kamanda wa Polisi Pwani Ulrich Matei alithibitisha kutokea ajali hiyo.
Akizungumza
hospitali hapo, Mganga Mkuu wa Hospitali ya hiyo, Dk Peter Dattan
alithibitisha kupokea baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo na kusema kuwa
kati ya 24 waliofikishwa hapo wawili walifariki na wote ni wanaume
majina yao bado hayajajulikana.
Dk Dattan
alisema majeruhi 22 wanaendelea kupatiwa matibabu na kati yao wanawake
ni 12 na kwamba kwa jumla hali zao wote ni mbaya kutokana na majeraha
makubwa waliyoyapata.
Naye
Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Chalinze walikolazwa majeruhi wengine Dk
,Victor Bamba akizungumza kituoni hapo alisema majeruhi waliofikishwa
hapo ni 12.
Alisema
majeruhi watatu kati ya hao walikuwa wakifanyiwa mpango wa kupelekwa
Tumbi baada ya hali zao kubadilika na kwamba wengi wao wameumia zaidi
sehemu za kichwani, kuvunjika miguu, mikono na mbavu
Dk Bamba
aliiomba Serikali na wadau wa afya kuhakikisha kuwa utoaji na usambazaji
dawa na vifaa tiba unalenga kwenye maeneo yenye ajali nyingi za
barabarani ili kuweza kupatikana dawa na vifaa tiba kwa wakati pindi
inapotokea matukio ya ajali.
Kwa
mujibu wa mashuhuda na wakazi wa Kijiji cha Kimange, Hamis Shaaban na
Yusufu Mzee walisema ajali hiyo ilitokea saa 5.40 asubuhi jana.
No comments:
Post a Comment