ANGALIA PICHA::JAMBAZI LANUSURIKA KIFO MBEZI JIJINI DAR
Jambazi likiwa hoi baada ya kichapo kutoka kwa wanachi.
Jambazi hilo likihojiwa.
Mmoja wa wanausalama (mwenye tisheti yenye mistari) akiwa na bastola aliyokutwa nayo jambazi huyo.
Wananchi wakiwa eneo hilo la tukio.
Wanausalama wakishauriana jambo kabla ya kulipiga pingu jambazi na kulipeleka hospitali.
Baada ya kichapo kikali jambazi lilipelekwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu.
KIJANA mmoja ambaye hajafahamika jina lake anayedaiwa kuwa ni jambazi
amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali eneo la Mbezi kwa
Msuguli jijini Dar es Salaam. Kijana huyo pamoja na mwenzake wakitumia
pikipiki walikuwa na silaha za moto tayari kwa kwenda kufanya uhalifu
lakini kabla mpango wao haujakamilika polisi waliingilia kati na kuanza
kupambana nao. Haikuwa kazi rahisi kuweza kumkamata jambazi huyo
kutokana na majibizano ya risasi kati yake na polisi. Baada ya jambazi
lililokuwa linaendesha pikipiki kuona mwenzake anaelekea kukamatwa
lilitokomea wakati mwenzake akiangukia mikononi mwa wananchi wenye
hasira kali waliomshushia kipondo cha nguvu. (PICHA NA GPL)
No comments:
Post a Comment