MANNING
Askari wa Marekani Bradley Manning alietoa taarifa muhimu kwa mtandao wa Wikileaks amehukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 35 jela na pia amefukuzwa jeshini.
Kabla ya hukumu hiyo waendesha mashtaka walitaka Manning apewe adhabu ya kifungo cha miaka zaidi ya 60 jela.
Waendesha mashtaka hao walidai kuwa askari huyo kijana mwenye umri wa miaka 25 alihatarisha maisha ya maafisa wa Idara za Ujasusi kwa kutoa siri hizo.
Mwezi Julai mwaka huu Manning alipatikana na hatia ya kufichua ripoti za siri zaidi ya laki saba, zilizohusu vita vya nchini Irak na Afghanistan, pamoja na kutoa kwa mtandao wa Wikileaks nyaraka nyeti za Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.
No comments:
Post a Comment