Pages

Monday, August 19, 2013

IGP MWEMA AKABIDHI UENYEKITI WA SARPCCO NCHINI NAMIBIA.


1Mkuu wa Jeshi la Polisi la Tanzania IGP Said Mwema akimkabidhi kitara Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga kama ishara ya kumkabidhi uenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) baada ya Tanzania kumaliza uongozi wake kwa kipindi cha mwaka mmoja.Makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa mkutano maalumu wa wakuu hao uliofanyika nchini Namibia.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia)
2Mkuu wa Jeshi la Polisi la Tanzania IGP Said Mwema akiongozwa na Askari wa Namibia kuingia katika ukumbi wa mkutano ambapo alitumia fursa hiyo kukabidhi uenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia)
3Mkuu wa Jeshi la Polisi la Tanzania IGP Said Mwema akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga baada ya kumkabidhi uenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO).(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia)
………………………………………………………………………..
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi,Windhoek Namibia.
Inspekta Jenerali wa Polisi wa Tanzania IGP Said Mwema amekabidhi uenyekiti wa Umoja wa wakuu wa majeshi ya Polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika SARPCCO baada ya kumaliza kipindi chake cha mwaka mmoja cha kuongoza umoja huo.IGP Mwema amekabidhi uongozi huo kwa Inspekta Jenerali wa Polisi wa Nchi ya Namibia Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga wakati wa mkutano mkuu maalumu wa viongozi hao uliofanyika jana katika jiji la Windhoek na kuhudhuriwa na Wakuu wa Polisi kutoka nchi wanachama pamoja na viongozi mbalimbali kutoka INTERPOL na SADC.

No comments:

Post a Comment