Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limetangaza dau la Sh100
milioni kwa mtu atakayewezesha kupatikana kwa taarifa za kundi la
uhalifu linalojihusisha na vitendo vya kuwamwagia maji baadhi ya watu
yanayodhaniwa ni tindikali.
Hatua hiyo inatokana na vitendo hivyo kushamiri maeneo mbalimbali nchini.
Kamanda
wa Polisi Kanda hiyo, Suleiman Kova, alisema vitendo hivyo havipaswi
kuvumiliwa na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kuwafichua watu
hao.
“Nimeamua
kuomba fedha hizi serikalini ili nimpe mtu atakayewezesha kupatikana kwa
taarifa hizo, hatimaye kukomesha vitendo hivi. Kemikali hii imekuwa na
madhara makubwa,” alisema Kova.
Hivi karibuni Mkurungezi wa Maduka ya Home Shopping Center,
Mfanyabiashara wa Lebonon na raia wawili wa Uingereza walimwagiwa maji
yanayodhaniwa ni tindikali.
Wakati
huohuo, polisi linamshikilia raia wa Uingereza kwa tuhuma za kukutwa na
nyara mbalimbali za Serikali zenye thamani ya zaidi ya Sh100 milioni,
vikiwamo vipande vinane vya meno ya tembo.
Kova
alisema mtuhumiwa huyo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Usafirishaji
Mizigo (TALL), alikamatwa juzi saa 2:00 usiku maeneo ya Mbezi Beach,
wilayani Kinondoni.
Alisema
alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na meno 20 na kucha 22 za Simba,
shanga mbalimbali zilizotengenezwa kwa meno ya tembo, Kasuku na nyara
nyingine ambazo hairuhusiwi kumiliki bila kibali.
Alisema
uzito wa nyara hizo ni kilo 25, walimkuta na mawe mbalimbali
yanayodhaniwa ni madini sambamba na ganda moja la bomu lenye ukubwa mita
130.
No comments:
Post a Comment