Ibrahim Boubacar Keita ana jazi ngumu ya kukarabati nchi ya Mali
Ibrahim
Boubacar Keita ameibuka mshindi wa uchaguzi mkuu nchini Mali huku
mpinzani wake akikubali kushindwa katika duru ya pili ya uchaguzi wa
urais.
Soumaila Cisse,amekubali kushindwa na mpinzani wake,aliyekuwa waziri mkuu Ibrahim Boubakar Keita.
Bwana Cisse aliyewahi kuhudumu kama waziri wa fedha amempongeza Keita kwa ushindi huo na kumtakia kila la kheri.
Bwana Keita, mwenye umri wa miaka 68, alihudumu kama waziri mkuu kutoka mwaka 1994 hadi 2000.
Mali
imekumbwa na vurugu kwa kipindi cha mwaka mmoja ikiwemo mapinduzi ya
kijeshi na kufuatiwa na harakati za jeshi la Ufaransa kuwaondoa
wapiganaji waliokuwa wameteka eneo la Kaskazini mwa nchi.
Hata hivyo hakuna matokeo rasmi yametolewa kufuatia duru ya pili ya uchaguzi iliyofanyika Jumapili.
Katika duru ya kwanza bwana Cisse alipata 19% dhidi ya bwana Keita aliyepata 40%
Bwana
Keita anayejulikana kama (IBK) – atakuwa na jukumu la kusimamia zaidi
ya dola bilioni 4 za msaada wa kigeni kwa taifa hilo ambalo uliahidiwa
kwa ukarabati wa nchi.
Umoja
wa mataifa umeanza kupeleka kikosi cha wanajeshi 12,600 kitakachokuwa
na jukumu la kudhibiti hali nchini Mali, huku wanajeshi wa Ufaransa
wakianza kuondoka.
Baada
ya duru ya kwanza ya uchaguzi Bwana Cisse alikuwa amelalamika kuwepo
visa vya rushwa au ununuzi wa kura huku kura zaidi ya laki nne
zikisemekana kuharibika.
Hata
hivyo, mahakama ya kikatiba ya Mali ilikataa madai hayo huku kiongozi wa
waangalizi wa Ulaya Louis Michel, akisifu uchaguzi huo kwa
ulivyoandeshwa kwa njia ya uwazi.
Mnamo
Jumatatu, waangalizi kutoka Muungano wa ulaya na muungano wa Afrika,
walisifu ambavyo duru ya pili ya uchaguzi ilivyoendeshwa.
‘Raia wa Mali wanapaswa kupongezwa kwa sababu kulingana na mimi ninavyoona, wanatii demokrasia,” alisema Michel.
Kabla ya uchaguzi huo Bwana keita aliahidi kuleta maridhiano nchini humo iwapo angechaguliwa.
Makubaliano
yaliyoafikiwa ili kuruhusu uchaguzi kuendelea katika eneo hilo la
kazkazini yanashinikiza serikali iliyochaguliwa kuanzisha mazungumzo ya
amani na waasi wa kundi la Tuareg katika kipindi cha miezi miwili.
KUTOKA BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment