Pages

Sunday, August 18, 2013

KEMIKALI AINA YA SALPHONIC ACID YAUZWA KAMA NJUGU MITAANI JIJINI DAR ES SALAAM.



Tindika ikiwa katika ndoo tayari kwa kuuzwa, uchunguzi umebaini kuwa bidhaa hii hatari huuzwa kiholela jijini Dar es Salaam.
 
http://1.bp.blogspot.com/-ZsGljS1yiWY/UfFm6J0afwI/AAAAAAAAj-w/ieNOJTOYUl0/s320/shopping+centre.jpgMfanyabiashara maarufu na Mmiliki wa maduka ya Home Shopping Center(HSC), Said Mohamed Saad, ameliwa kwa kumwagiwa tindikali. 
Rais Jakaya Kikwete akimjulia hali Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhili Soraga.

SIKU chache baada ya wasichana wawili raia wa Uingereza kumwagiwa tindikali mjini Zanzibar, imebainika kuwa, tindikali za aina mbalimbali zinauzwa kiholela kama njugu jijini Dar es Salaam.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili unaonyesha kuwa jijini Dar es Salaam yapo maduka mengi yanayouza tindikali ya kila aina na bidhaa hiyo inauzwa bila ya udhibiti wowote kuanzia Kariakoo hadi Vingunguti.
Wiki iliyopita, Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele alitoa miezi mitatu kwa wafanyabiashara wa tindikali kujisajili ili kuzuia kuongezeka kwa matukio ya uhalifu kwa kemikali hiyo nchini.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika mitaa ya Dar es Salaam, umebaini kuwa tindikali za aina mbalimbali zinapatikana kwa wingi katika maduka ya rejareja na jumla, huku wauzaji wa bidhaa hizo wakishindwa kutoa tahadhari yoyote kwa wateja wao.
Imebainika kuwa tindikali zinazopatikana kwa urahisi zaidi ni Sulphonic Acid ambayo imetajwa kutumika kutengeneza sabuni za maji (multipurpose detergents), Sulfuric acid inayotumika kutengeneza maji ya betri na Hydrochroric acid inatumiwa na wajasiriamali kutengeneza dawa za usafi.
Kemikali nyingine ambayo imeelezwa na watumiaji wake kuwa ni hatari ni Hydrogen Peroxide ambayo hutumika kusafisha mafuta ya mawese yanayotumika kutengenezea sabuni za kipande.
Katika Mtaa wa Gerezani Kariakoo, kuna duka maalumu la kuuza kemikali mbalimbali kwa bei ya rejareja na jumla, kemikali hizo zinauzwa kati ya Sh4,000 hadi Sh6,000 kwa kilo moja kutokana na aina yake.
Muuza kemikali mmoja katika mitaa ya Sinza wilayani Kinondoni, ambaye hakutaka kutaja jina lake gazetini kuhofia usalama wake, alisema biashara hiyo ilianza kushamili miaka mitatu iliyopita baada ya kuanzishwa kwa mafunzo ya kutengeneza bidhaa mbalimbali zinazotumia kemikali.
“Matangazo yanayotolewa katika vyombo vya habari kuhusu ujasiriamali wa kutengeneza sabuni aina mbalimbali, ndiyo yaliyochochea kuongezeka kwa mahitaji ya tindikali hapa nchini. 


Kwa mfano, (anamtaja mhusika) anafundisha namna ya kutengeneza maji ya betri za magari kwa kutumia Sulphuric acid, unategemea wajasiriamali wakanunue wapi hiyo tindikali?” anahoji.
Matukio ya kujeruhiwa na tindikali.
Agosti 7 mwaka huu raia wawili wa Uingereza, Kate Gee na Kirstie Trup wote miaka 18 walishambuliwa kwa tindikali na watu wasiojulikana wakati wakitembea kwenye mitaa ya Stone Town mjini Zanzibar. Raia hao walisafirishwa na kurudishwa Uingereza ambako wanaendelea na matibabu.

Kabla ya kuondoka nchini, Rais Jakaya Kikwete aliwatembelea raia hao hospitali na kusema kuwa tukio hilo limeitia aibu nchi kwa mataifa ya nje na kuliamuru Jeshi la Polisi kuhakikisha linawakamata na kuwafungulia mashtaka wote waliohusika. MWANANCHI.

No comments:

Post a Comment