Pages

Saturday, August 24, 2013

LIGI KUU TANZANIA:::COASTAL UNION YAIPIGA JKT OLJORO 2 KWA NUNGE

 Mashabiki wa Coastal Union.... kuna mtu namfananisha hapa sijui ni nani... Kwa jaaaam.

                                               Morocco kama Mourinho vile...

                                           Jamani Kado muda si mrefu atarudi timu ya Taifa.

                                        Haruna leo alijitoa mhanga sana.... Kaupiga mwingi.

 Huyu Marcus Ndehele akisalimiana na kocha wake wa zamani wa Oljoro JKT, Fikiri Elias.

           Said Lubawa naye akisalimiana na afande mwenzie wa zamani baada ya mchezo kuisha.


Hatimaye vijana wa Coastal Union wamefanya walichoagizwa na mwalimu wao Hemed Morocco baada ya kuwatandika Oljoro JKT mabao 2-0.

Katika mchezo huo ambao kwa upande mmoja unaweza kusema Oljoro hawakuwa tayari kucheza ama walilazimishwa kwa namna walivyokuwa wanapoteana dimbani mpaka kuruhusu mabao mawili ambapo moja limetokana na makosa ya golikipa na la pili ni kosa la beki.

Hata hivyo wana Mangush walishindwa kutumia vema nafasi walizopata baada ya kukosa mabao takriban manne kwa vipindi vyote ambapo Selembe peke yake amekosa mabao mawili, Yayo amekosa bao moja na Odula pia amekosa moja.

Abdi Banda ndiye aliyeanza kuipa furaha Coastal Union ndani ya dakika ya 11 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Selembe akiwa umbali mdogo tu kutoka mstari wa kati ya uwanja winga ya kushoto, akamwangalia golikipa amekaa upande gani akafanya kama anapiga krosi mpira ukatumbukia moja kwa moja wavuni.

Baada ya hapo JKT Oljoro walibadilika kidogo wakafanya mashambulizi ingawa hayakudumu sana, Coastal Union wakaanza kujipanga upya na kuendeleza jaramba. Ilipotimia dakika ya 35 ulipigwa mpira wa adhabu kuelekea langoni mwa Oljoro baada ya Hamad Juma kuchezewa madhambi, mchezaji wa Oljoro akawa anajaribu kuokoa lakini mpira ukambabatiza usoni Crispian Odula ukatumbukia wavuni katika dakika ya 36.

Mpaka mwamuzi wa leo Jacob Adengo kutoka Mwanza anapuliza kipyenga kuashiria mpira ni mapumziko matokeo yalisomeka Coastal Union 2-0 Oljoro JKT.

Kipindi cha pili kilianza kwa kusomana timu zote mbili mpaka dakika ya 50 ambapo Wagosi waliendelea kulisakama lango la maafande hao bila huruma. Lakini wagosi bahati haikuwa yao kwani waligosi amabao mengi sana ya wazi. Hata hivyo golikipa Shaaban Kado aliokoa michomo mingi sana.

Ilipofika dakika ya 21 kipindi cha pili kocha Morocco alifaya mabadiliko ambapo alimuingiza Masumbuko Keneth akamtoa Uhuru Suleiman. baadaye dakika ya 35 kipindi cha pili alitolewa Selembe akaingia Pius Kisambale na ilipofika dakika ya 44 muda mchache kabla ya kipyenga cha mwisho kupulizwa alitoka Crispian Odula akaingia Mohammed Sudi.

Kocha Morocco anasema hizi ni salamu kwa wana jangwani jumatano wiki ijayo atakapokutana nao uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha leo ni:
1. Shaaban Kado.
2. Hamad Juma.
3. Abdi Banda.
4. Marcus Ndehele.
5. Juma Nyoso.
6. Razak Khalfan.
7. Uhusu Suleiman.
8. Haruna Moshi.
9. Kato Yayo.
10. Crispian Odula.
11. Suleiman Kassim ‘Selembe’.

Sub: Said Lubawa, Mbwana Kibacha, Othaman Tamim, Pius Kisambale, Masumbuko Keneth, Yusuf Chuma na Mohammed Sudi.


COASTAL UNION
24 AGOSTI, 2013
ARUSHA, TANZANIA

No comments:

Post a Comment