Arsenal imeibamiza klabu ya Fenerbahce ya Uturuki goli 3 bila katika pambano kali la kusisimu kuwania nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Arsenal ambayo wikiend iliyopita ilibamizwa na Aston Villa 3-1 katika Ligi kuu England ilisafiri mpaka katika Jiji la Instanbul Uturuki kuikabili Fenerbahce huku mashabiki wengi wakiamini kuwa Arsenal ingepoteza mchezo huo baada ya kukabiliwa na majeruhi wengi na kutosajili msimu huu.
Lakini vijana wa Wenger walitulia na kuudhihirishia Ulimwengu kama Arsenal ni timu kubwa na itaendelea kubaki kuwa kubwa baada ya kucheza mchezo mzuri na kufanikiwa kupata ushindi huo mnono ugenini.
Arsenal walipata goli la kwanza kupitia kwa beki wake Kieran Gibbs baada ya kuunganisha krosi ya Theo Walcott kabla ya Aaron Ramsey hajafunga goli la pili kwa shuti kali huku Olivier Giroud akimalizia la tatu kwa kufunga penalti baada ya Walcott kufanyiwa madhambi na kufufua matumaini ya kusonga mbele watakaporudiana wiki ijayo katika uwanja wa Emirates.
Katika michezo mingine ya kombe hilo iliyopigwa usiku wa jana ilishuhudia Schalke 04 ya Ujerumani akibanwa na kutoa sare ya 1-1 na PAOK FC
Usiku huo pia ulishuhudia FC Basel ya Uswis Ikishinda 4-2 dhidi ya PFC Ludogorets Razgard ugenini.
Dinamo Zagreb ilikubali kichapo cha 2-0 nyumbani toka kwa Austria Wien wakati Steaua Bucuresti ikilazimishwa sare na Legia Warszawa.
Mechi za marudiano zitachezwa Jumanne Ijayo ambapo washindi wataingia katika makundi ya Kombe hilo ambalo linaaminika kuwa tajiri kwa upande wa Vilabu duniani.
No comments:
Post a Comment