Pages

Saturday, August 31, 2013

Makuli zaidi ya 400 wa bandari ya Mwanza wagoma


  
Makuli zaidi ya 400 wa bandari ya Mwanza wamegoma kupakia na kupakua shehena ya mizigo kutoka ndani ya meli ya Mv. Victoria na meli zingine zinazotoka nje ya nchi zinazoegeshwa katika bandari ya mwanza kusini baada ya uongozi wa mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania( TPA) Mwanza kusitisha zabuni ya ubebaji wa mizigo unaofanywa na makuli hao katika bandari  zake .
Mgomo huo ambao umeanza leo asubuhi na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wafanyabiashara wanaotumia bandari hizo mbili,umetokana na hatua ya uongozi wa mamlaka ya bandari Tanzania(TPA)  - Mwanza kusitisha mkataba wa zabuni ya upakiaji na upakuaji wa mizigo katika meli zinazomilikiwa na mamlaka hiyo, kwa barua iliyosainiwa na Bw. Ngowi kwa niaba ya mkuu wa bandari ya Mwanza yaagosti 19 mwaka huu.
Makuli hao ambao pia ni wana ushirika wakiongozwa na mwenyekiti wa ushirika wa wahudumu wa bandari ya mwanza kaskazini na kusini Bw. Rajab Said, wamepinga kitendo cha kucheleweshwa kutangazwa kwa zabuni na kisha kupewa nyongeza ya mwezi mmoja kuendelea na shughuli za upakiaji na upakuaji kwa bandari zote mbili, na wakati huo huo Mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania kutangaza zabuni nyingine mpya ni kitendo kinachoashiria kuwanyanyasa wanaushirika hao na hivyo wamemuomba waziri wa uchukuzi Mh. Dk.Harrison Mwakyembe kuingilia kati suala hilo ili kuwabaini baadhi ya viongozi wanaotaka kujinufaisha na zabuni hizo
Itv imeshuhudia baadhi ya wafanyabiashara wakiwa katika pilikapilika za upakuaji wa mizigo yao, ikiwemo mikungu ya ndizi na magunia ya maparachichi iliyowasili leo asubuhi kwa meli ya Mv. Victoria ikitokea Bukoba kupitia bandari ya Kemondo baada ya makuli ambao wamekuwa wakifanya kazi hiyo siku zote kugoma kuingia kazini, huku baadhi yao wakilalamikia kitendo hicho kwamba kimewasababishiausumbufu mkubwa ikiwemo kuharibika kwa matunda yao ya ndizi mbivu.
Kaimu mkuu wa bandari ya Mwanza Bw. Kasyupa alipotafutwa na Itv ili kuzungumzia mgomo huo hakuweza kupatikana ofisini kwake,lakini itv imefanikiwa kupata mojawapo ya barua aliyowaandikia viongozi wa ushirika huo, ikieleza kuwa shughuli za kupakia na kupakua shehena bandarini zitaendeshwa na mamlaka ya usimamizi wa bandari tanzania yenyewe mpaka hapo itakapotangazwa utaratibu wa zabuni.na ITV

No comments:

Post a Comment