Manchester United wamatuma ofa nyingine ya pamoja ya £35 million kwa ajili ya wachezaji wa Everton Marouane Fellaini na Leighton Baines mapema leo, taarifa kwa mujibu wa Telegraph.
Ofa hiyo mpya imegawanyika kwa £20m kwa ajili ya Maroune Fellaini na £15m kwa ajili ya Leighton Baines, hii inakuja baada ya Toffees kuikataa ofa ya mwanzo ya £28m.
Kocha wa Everton Roberto Martinez amekuwa akikaririwa akisema angependa kuendelea kuwa na wachezaji hao Goodison Park lakini mhispania huyo anataka hatma ya wachezaji hao ijulikane mapema ili aweze kufanya maamuzi ya kuimarisha kikosi chake kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.
Pia kocha huyo wa zamani wa Wigan amesema wachezaji wake hao wawili sasa wnaonekana kutokuwa sawa kisaikolojia kutoka na kutakiwa huko na United hivyo kushindwa kuweka umakini wao katika kuitumikia klabu yao.
Kocha wa United David Moyes ni shabiki mkubwa wa Fellaini na Baines, ambao amefanya kzi kwa muda mrefu ndani ya Everton kabla hajaenda Old Trafford kumrithi Sir Alex Ferguson
No comments:
Post a Comment