Msemaji
wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bw. Gaston Makwembe KUSHOTO
akiwaeleza waandishi wa habari Mpango wa Halmashauri kujenga vituo vya
Mabasi yaendayo mikoani na nchi za jirani katika maeneo ya Mbezi Luis na
Boko Basihaya katika mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es
Salaam KULIA ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.
Meneja
wa Kituo cha Mabasi Ubungo Bw. Juma Iddi KUSHOTO akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari juu ya ushiriki wao katika utoaji wa huduma ya
usafiri wa Mabasi yaendayo haraka(Dar Rapid Transit-DART) katika mkutano
na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam KULIA ni Msemaji wa
Halmashauri hiyo Bw. Gaston Makwembe.
PICHA NA ELIPHACE MARWA.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Halmashauri
ya Jiji la Dar es Salaam itajenga vituo vya mabasi yaendayo mikoani na
nchi za jirani katika maeneo ya Mbezi Luis na Boko Basihaya. Ujenzi wa
vituo hivyo ni utekelezaji wa mipango ya Jiji ya kuimarisha huduma za
usafiri Dar es Salaam. Kituo cha Mbezi Luis kitahudumia wasafiri wa
Kanda ya Kati na Nyanda za Juu wakati Kituo cha Boko Basihaya kitatoa
huduma kwa wasafiri wa Kanda ya Kaskazini. Kwa Kanda ya Kusini
Halmashauri ya Jiji itajenga Kituo cha Mabasi Kongowe.
Kituo
kitakachoanza kujengwa ni Mbezi Luis ambacho kitajengwa sambamba na
Boko Basihaya. Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo kimepangwa kutoa huduma ya
usafiri wa mabasi yaendayo haraka kwa wasafiri wote watakaokuwa
wakitumia vituo hivyo vya mabasi yaendayo mikoani. Ujenzi wa vituo vya
Mbezi Luis na Boko Basihaya, kutokana na upembezi yakinifu wa awali,
unakadiriwa kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 40 kwa kila kituo.
Ujenzi
wa vituo hivyo unahitaji upembuzi yakinifu wa kina kwa lengo la kupata
gharama halisi za utekelezaji wake, kubaini vyanzo vya fedha na
kuangalia uwezekano wa kuzishirikisha taasisi mbalimbali za fedha na
wawekezaji wanaoonyesha nia ya kushirikiana na Halmashauri ya Jiji
katika ujenzi wa vituo hivyo ambavyo vitakapokamilika vitakuwa pia ni
chanzo cha ajira kwa wananchi.
Katika
kipindi hiki cha maandalizi ya ujenzi wa vituo hivyo, bado Kituo Kikuu
cha Mabasi Ubungo (UBT) kitaendelea kutoa huduma kwa wasafiri waendao
mikoani na nchi za jirani. Halmashauri ya Jiji inapenda wananchi
wafahamu kwamba UBT, kama ilivyopangwa na Serikali, itakuwa ni kituo
kitakachotoa huduma ya usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka(Dar Rapid
Transit-DART) baada ya kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu yake. Pamoja
na hilo Halmashauri ya Jiji pia itajenga “shopping malls” na hoteli
katika kituo hicho cha UBT
Kukamilika
kwa ujenzi wa vituo hivyo vya mabasi ni mafanikio makubwa katika
jitihada za serikali za kuimarisha huduma za usafiri katika Jiji la Dar
es Salaam. Wadau wa maendeleo katika sekta hii, wananchi na taasisi
mbalimbali wanategemewa kuendelea kutoa mapendekezo yao ya kuimarisha
huduma za usafiri Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment