Pages

Wednesday, August 21, 2013

MZUMBE NA TUMAINI KUIPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA BUNGE LA VIJANA MALAWI


1Hawa ni Bwana Joseph Lyimo mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe (kulia) na Bi. Zuwena Ibrahim mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini ambao wamechaguliwa kuiwakilisha Tanzania katika Bunge la vijana kutoka mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) litakalofanyika Lilongwe, Malawi kuanzia tarehe 21 hadi 26 Agosti 2013 ambapo pamoja na mambo mengine watazungumzia umuhimu wa kuwashirikisha vijana mapema katika vyombo vya maamuzi.

2Rais wa CPA Kanda ya Afrika na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (Mb), akiwakabidhi Waheshimiwa Wabunge hao wateule bendera ya Tanzania akiwataka waiwakilishe na kuipeperusha vema bendera hiyo ya Tanaznia katika Bunge la Vijana. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Naibu Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb),  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Mhe. Mussa Zungu Azzan, (Mb) na Kamishna wa Bunge Mhe. Beatrice Shilukindo (Mb).
3Wahadhiri waandamizi kutoka katika Vyuo Vikuu vya Mzumbe na Tumaini walioambatana na wanafunzi wao katika hafla ya kuwaaga. Hapa wapo kwenye picha ya pamoja na Mhe. Spika Makinda.4Spika Makinda akimpa mkono wa heri na baraka Mhe. Zuwena kama ishara ya kuwaaga vijana hao5Mhe. Joseph Lyimo akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya hafla hiyo ambapo ameahidi kuiwakilisha Tanzania vema.
 Na Prosper Minja – Bunge

No comments:

Post a Comment