HAPA NDIPO MAREHEMU ALIPOGUSA NA KUKUTWA NA MAUTI
NYAYA
ZA UMEME AMBAZO ZIMENING'INIA MITA MOJA KUTOKA USAWA WA ARDHI
ZIMESABABISHA KIFO CHA NEEMA B. KIPENYA (26) ALIPOTELEZA NA KUKAMATA
NYAYA HIZO KISHA KUFARIKI PAPO HAPO.
KATI
YA NGUZO HADI NGUZO NI UMBALI WA ZAIDI YA MITA 75 MAHALI AMBAPO
PALIPASWA KUWA NA NGUZO TATU LAKINI IKAWEKWA NGUZO MOJA , HALI MTEJA WA
ENEO HILO ALIKUWA AMELIPIA NGOZO TATU ZAIDI YA MIAKA MIWILI ILIYOPITA .
HAPA NDIPO ALIPO TELEZA MAREHEMU NEEMA NA KUANGUKIA NGUZO HIZO
ASKARI AKIPATA MAELEZO KUTOKA KWA MASHUHUDA
MWENYEKITI
WA KIJIJI CHA MSHIKAMANO BWANA KISMAN MWANGOMALE AMBAYE NDIYE MTEJA WA
KWANZA KULIPIA TANESCO NGUZO TATU NA KUFUNGWA NGUZO MOJA , NA AMETOA
TAARIFA MARA KADHAA TANESCO NA HATA KUANDIKA BARUA KWA NIABA YA KIJIJI
LAKINI HAKUNA UTEKELEZAJI ULIOFANYIKA HADI MADHARA YAMETOKEA NDIPO
TANESCO WAMEFIKA.
MMOJA
KATI YA WATUMISHI WA TANESCO AMBAYE ALIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUKATA
UMEME USILETE MADHARA ENEO HILO , HATA HIVYO ALINUSURIKA KUPIGWA NA
WANANCHI WENYE HASIRA KALI AMBAO WALIKERWA NA TUKIO HILO.
MWENYEKITI
WA KIJIJI CHA MSHIKAMANO WA KWANZA KUSHOTO NA WATUMISHI WA TANESCO
WAKIANGALIA NGUZO ZILIZO ELEMEWA NA UZITO WA NYAYA HIZO NA KUSABABISHA
NGUZO KUSHINDWA KUHIMILI UZITO WA NYAYA HIZO.
WAOMBOLEZAJI WAKILIA KWA UCHUNGU KWANI MUDA MFUPI ULIOPITA WALIKUWA NA MAREHEMU NYUMBANI HAPO.
MOJA KATI YA NDUGU AMBAYE ALIZIRAI KATIKA ENEO LA TUKIO
MWILI
WA MAREHEMU UKIWA KATIKA CHUMBA CHA MAITI HOSPITALI YA IFISI ILIYOKO
WILAYA YA MBEYA UKISUBIRI UCHUNGUZI ZAIDI WA KITABIBU.
PICHA NA EZEKIEL KAMANGA
NA MBEYA YETU BLOG
FUATILIA
KESHO JE TANESCO WATAREKEBISHA NGUZO HIZO? HII NI SINTO FAHAMU .. NB:
TATIZO KAMA HILI LIPO WILAYANI CHUNYA NI MIEZI MITATU TANGU LITOLEWE
TAARIFA TANESCO WILAYA YA CHUNYA NA MKOANI, LAKINI HADI LEO HAKUNA
KILICHOFANYIKA NA NYAYA HIZO HAZINA GAMBA LA PLASTIC(INSULATOR). MENEJA
AKILI KUPOKEA TAARIFA HIZO NA KUAHIDI KUFANYIA KAZI.
No comments:
Post a Comment