SHAHIDI
wa tano katika kesi ya kutorosha wanafunzi inayomkabili Mchungaji wa
Kanisa la TAG, raia wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC), Jean Felix
Bamana ameieleza mahakama namna alivyolazimishwa kufanya mapenzi na
mchungaji huyo.
Shahidi
huyo, Angela Swai (19), akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu, Naomi
Mwerinde wa Mahakama ya Hakimu mkazi Moshi, alisema Mchungaji huyo
alimlazimisha kufanya kitendo hicho jaribio ambalo lilishindikana
kutokana na mshitakiwa huyo kukataa kutumia kondomu.
Akiongozwa
na mwendesha mashtaka, wakili wa serikali, Esther Majaliwa, katika
ushahidi wake, Shahidi huyo alieleza Mahakama hiyo alivyokutana na
mshtakiwa kwa mara ya kwanza na mara ya pili ambapo alisema alikutana
naye kupitia marehemu mama yake mzazi huku mara ya pili akikutana naye
kupitia mtandao wa kijami.
Shahidi
huyo alieleza mahakamani hapo kuwa alikutana na mshtakiwa kwa mara ya
kwanza kupitia mama yake na alimtambulisha yeye na mdogo wake aliyemtaja
kwa jina la Arthur kuwa mchungaji huyo ni baba yao mwingine na
waliendelea kufahamiana kwani alikuwa ni rafiki mkubwa wa mama na
mshirika wake katika Biashara ya Madini.
Alisema
kwa kipindi kirefu hakuwahi kumuona hadi alipokutana naye kwa mara ya
pili mwaka jana kupitia mtandao wa Facebook ambapo alimwomba urafiki kwa
nia njema kwani alikuwa ni rafiki mkubwa wa marehemu mama yake, na
kuongeza kuwa mawasiliano yalikuwa ni ya kawaida tu.
Shahidi
huyo alisema baada ya hapo mshtakiwa alianza kumsisitiza kuhamia Dar es
Salaam kwa ahadi ya kumsaidia kuendelea na masomo baada ya kumueleza
amefukuzwa shule jambo ambalo yeye binafsi alilikataa.
Alisema
baada ya kukataa kukubaliana na wazo la kwenda Dar es Salaam, mshtakiwa
huyo alimwambia atafika Moshi ambapo alifikia katika Hoteli ya Moshi
View, Februari 14, mwaka huu na kufanya naye mawasiliano kupitia simu ya
mdogo wake aliyetajwa mahakamani hapo kwa jina la Arthur Swai, akimtaka
kumfuata hotelini hapo
No comments:
Post a Comment