Katibu
wa Shura ya Maimamu, Sheikh Ponda Issa Ponda (pichani kushoto) leo
ametoka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha mifupa
(MOI) alikolazwa kwa tiba ya jeraha la kinachosemekana kuwa ni risasi na
kusemekana amepelekwa katika gereza ambalo halijatajwa.
Msemaji
wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Bw. Almasi amethibitisha hilo na
kusema madaktari walimruhusu Sheikh Ponda bakutoka wodini baada ya hali
yake kiafya kuimarika na kuonekana hana sababu ya kuendelea kubaki
hapo.
Kuhusu
habari kuwa alipigwa risasi, Bw. Almasi amesema Muhimbili walimpokea
Sheikh Ponda akiwa na kidonda ambacho kilihudumiwa sehemu ingine kabla
ya kupelekwa hna kwamba hawakumkuta na risasi mwilini mwake. Badala
yake, alisema, walikifungua upya kidonda hicho na kukihudumia upya.
No comments:
Post a Comment