Mshindi
wa kwanza katika mbio za mita 10000 kwa Wanaume Fabian Nelson
(Tanzania) katika Michezo ya Umoja wa wakuu wa Polisi kwa Nchi za kusini
mwa Afrika (SARPPCO) Nchini Nambia akishangilia na bendera ya taifa
mara baada ya kumaliza mbio hizo katika uwanja wa taifa wa Namibia
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia).
Mshindi
wa kwanza katika mbio za mita 10000 kwa Wanaume Fabian Nelson
(Tanzania) akivalishwa medali ya dhahabu na mmoja wa makamishna wa
Polisi wa Namibia katika Michezo ya Umoja wa wakuu wa Polisi kwa Nchi za
kusini mwa Afrika (SARPPCO) katika uwanja wa taifa wa Namibia (Picha
na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia)
Baadhi
ya wanamichezo wa Tanzania wakishangilia ushindi wa kwanza katika mbio
za mita 10000 kwa Wanaume katika Michezo ya Umoja wa wakuu wa Polisi kwa
Nchi za kusini mwa Afrika (SARPPCO) katika uwanja wa taifa wa Namibia
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia).
Wanariadha
wa Polisi Tanzania katika mbio za mita 10000 kwa Wanaume Wilbrado Peter
wa kwanza na Fabian Nelson wakikimbia katika Michezo ya Umoja wa wakuu
wa Polisi kwa Nchi za kusini mwa Afrika (SARPPCO) Nchini
Nambia.Fabiana Nelson aliongoza mbio hizo akifuatiwa na Wilbrado Peter.
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia)
Wanariadha
wa mbio za mita 10000 kwa Wanaume wakikimbia katika Michezo ya Umoja wa
wakuu wa Polisi kwa Nchi za kusini mwa Afrika (SARPPCO) Nchini
Nambia.. (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia).
WANARIADHA WAANZA KUIPA MEDALI POLISI TANZANIA NCHINI NAMIBIA.
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi,Windhoek Namibia.
Wanariadha
wanaowakilisha Jeshi la Polisi Tanzania katika michezo ya Umoja wa
wakuu wa Polisi kusini mwa Afrika SARPCCO nchini Namibia wameanza vyema
mbio hizo baada ya kufanikiwa kunyakua medali za Dhahabu na fedha katika
mbio za mita elfu 10000 wanaume.
Aliyenyakua
medali ya dhahabu ni Mwanariadha Fabian Nelson ambaye alitumia dakika
30 na sekunde 42 huku akifuatiwa na Wilbrado Peter (Tanzania) ambaye
alitumia dakika 30 na sekunde 45 na kuwaacha wanariadha wengine nyuma
kutoka mataifa ya Zimbabwe,Namibia,Botwasana na Angola.
Wengine
walioipatia Tanzania Medali ni pamoja na Basili John mita 800 (Shaba )
na Mohamed Ibrahim mchezo wa kurusha kisahani (shaba).
Katika
mpira wa miguu mechi ya ufunguzi ilizikutanisha wenyeji Namibia na
Msumbiji ambapo Namibia iliichapa Msumbiji mabao 2 kwa 0 huku kwenye
mpira wa miguu wanawake Namibia na Angola zilitoka suluhu ya bila
kufungana.
Tanzania
itaanza kutupa karata yake katika mpira wa miguu dhidi ya Zambia ambapo
Tanzania imepangwa kundi B ikiwa na timu za Zambia, Angola ,DRC na
Lesotho huku Kundi B lina timu za Namibia, Msumbiji, Botswana na
Zimbabwe.
No comments:
Post a Comment