Pages

Wednesday, August 21, 2013

UTOZAJI WA USHUHURU WA MAGARI COCO BEACH,JE HALMASHAURI YA KINONDONI MNAHUSIKA AU HAMJUI?


 Na www.sufianimafoto.com
Mfanyakazi wa Inayojiita kampuni ya kukusanya Ushuru ya MTAA WA OYSTERBAY BEACH PARKING, ambaye hakutaka kutaja jina lake akiandika risiti ya ushuru wa maegesho ili kuweka katika moja ya gari lililokuwa katika ufukwe wa Coco Beach, ili alipwe ushuru wa maegesho hayo kiasi cha Sh. 1000 kila gari. Mfanyakazi huyo alipohojiwa na mtandao huu alisema kuwa anauwezo wa kukusanya hadi magari 20 kwa siku jambo ambalo si la kweli kwani kwa muda mchache tu alishapitia magari zaidi ya hayo.

Na alipoulizwa zinapopelekwa fedha hizo baada ya kukusanywa alisema ''Mimi sijui zinapopelekwa kwani mimi ni mfanyakazi tu na nikishakusanya nampelekea Bosi ndo anajua zinapokwenda, kwa siku naweza kukusanya ushuru hadi wa magari kama 15 hivi,kwa sababu sipo peke yangu tupo wengi katika eneo hili lote''. alisema mfanyakazi huyo.

Hata hivyo baadhi ya watu waliokuwapo ufukweni hapo, walisikika wakin'gaka kutoa ushuru huo, huku wakimhoji ''Tutoe ushuru wa Parking kwa lipi, hata usafi tu hamfanyi nyie mnajua kuchukua hela tu, na kwanza mlishazuiliwa kukusanya pesa hizi bado tu mnaendelea na wizi wenu''. alisikika akilalama jamaa mmoja

Imeelezwa kuwa Kampuni hiyo inayojishughulisha na kukusanya ushuru huo, ilishawahi kuwa na mgogoro kipindi cha nyuma, ambapo wahusika waliwahi kukamatwa na kufikishwa hadi Kituo cha Polisi na kuzuiliwa kufanya kazi hiyo, kutokana na kutokuwa na ruhusa ya kufanya hivyo na kwamba hawatambuliki na Halmashauri wala serikali, lakini wanaendelea kinyemela na kufanya baadhi ya watu wanaowafahamu kuwagomea kutoa ushuru huo wanapofuatwa kulipia parking hiyo.

Na hata ukiitazama kwa makini Risiti hii haionyeshi Adress kamili ya wahusika, haina mhuri wala namba za simu zaidi ya kuandika jina la Serikali ya Mtaa wa Oysterbay Beach, Sasa kuna kila haja ya kuwahoji Viongozi wa Serikali ya Mtaa huo ili kujua Mapato na Matumizi ya ukusanyaji wa Ushuru huu, unaokusanywa kuanzia Jumatatu hadi Jumapili bila kupumzika na zinapokwenda Fedha hizo. 
 Hii ndiyo Risiti yenyewe inayotolewa baada ya kutoa Sh. 1000 kwa mkusanyaji, ambaye pia anakuwa ameambatana na vijana wawili waliovalia kiraia Jinzi na Tisheti na makofia ya Sweta, wakimlinda mkusanyaji huyu mdada na kupiga mkwara kwa anayeonekana kukaidi kutoa Buku.
 Mkusanyaji akiandika Risiti hiyo, ambayo hata akiisha ichana haibaki Kopi yake kuonyesha kilichoandikwa, Yaani ni Vishina kwa kwenda mbele.
 Akienda kuweka risiti  katika gari
 Akitimiza wajibu wake kuweka katika gari....
Huyu ndiye mkusanyaji wa ushuru katika Fukwe hiyo.

No comments:

Post a Comment