Pages

Saturday, August 24, 2013

WANAHABARI IRINGA WATANGAZA KUMALIZA MGOGORO NA JESHI LA POLISI IRINGA

KamuhandaRuvuma_d5905.jpg
RPC MICHAEL KAMUHANDA (ALIYEHAMISHWA)
KLABU ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) imetangaza rasmi kumaliza mgogoro na jeshi la polisi baada ya aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda kuondolewa mkoani hapo na nafasi yake kuchukuliowa na kamanda mpya Ramadhan Mungi.
P.T

Mwenyekiti wa IPC Frank Leonard ametoa tamko hilo la kumaliza mgogoro na jeshi la polisi mkoa wa Iringa ,leo katika mkutano mkuu maalum wa UTPC uliomalizika leo katika ukumbi wa Hotel ya Gorden Hotel mjini Dodoma.
rpc_iringa_2_1febd.jpg
RPC MPYA IRINGA BW.RAMADHAN MUNGI
Bw Leonard alisema kuwa hatua ya IPC kutoa tamko hilo ilikuja baada ya Kamuhanda kuhusishwa na kifo cha Daudi Mwangosi aliyekuwa mwenyekiti wa IPC .
" Ndungu wajumbe wa UTPC napenda kuwatangazia sasa kuwa mgogoro wetu na jeshi la polisi Iringa umemalizika baada ya RPC Kamuhanda kuhamishwa mkoani Iringa na sasa tunaendelea kufanya kazi na jeshi la polisi Iringa"
Siku ambayo aliyekuwa mwenyekiti wa IPC marehemu Daudi Mwangosi alipouwawa katika kijiji cha Nyororo wilaya ya Mjufindi ilikuwa ni septemba 2 /2012 siku ya jumapili majira ya saa 10 jioni.
Na Francis Godwin

No comments:

Post a Comment