Tunashauriwa kunywa maji ya kutosha ili kuwa na afya njema. Sehemu kubwa ya mwili wako ni maji. Kila seli kwenye mwili wako unahitaji maji ili kuchukua chakula na kutoa uchafu. Pia maji yanahitajika kwa usafirishaji mwilini, sehemu kubwa ya damu ni maji. Faida hizo zimezungumzwa sana na hivyo umesisitizwa kunywa maji walau lita moja na nusu kwa siku ili kuwa na afya njema. Kuna faida nyingine za maji ambazo huwa hazizungumziwi sana, na hizihapa ni baadhi tu ya faida hizo
1. Kunywa
maji kwa wingi kunakufanya uonekane kijana. Mwili wako ukiwa na maji ya
kutosha inazuia ngozi kukunjamana na hivyo mtu kuonekana na ngozi
nyororo hata kama umri umekwenda.
2.
Kupunguza uzito/unene. Kama hupendezwi na uzito ama unene wa mwili wako
ukinywa maji mengi utapunguza uzito wako. Unywaji wa maji mengi
unapunguza uzito wa mwili kwa sababu;
Ukinywa
maji mengi unapunguza hamu ya kula hivyo hutoweza kula chakula kingi
kinachosababisha uzito kuwa mkubwa. Pia maji yanasaidia uunguzwaji wa
mafuta mwilini na kusidia kuondoa sumu mwilini.
3.
Kujenga misuli. Mwili unapokuwa na maji ya kutosha unaweza kusambaza
hewa ya oksijeni vizuri zaidi na hivyo misuli ya mwili inaweza kufanya
kazi kwa muda mrefu bila kuchoka. Hii inasaidia kujenga misuli ya mwili.
4.
Kuongeza akili, ndio unywaji wa maji unaongeza uwezo wa kufikiri na
kuweka kumbukumbu. Hii ni kwa sababu maji yanasambaza chumvi
zinazohitajika na seli za fahamu kwa ajili ya kusafirisha taarifa
mbalimbali. Tafiti zinaonyesha kwamba ukinywa glasi 10 za maji unaongeza
uwezo wa kufikiri kwa asilimia 30. Jaribu kama huamini.
5.
Unywaji wa maji mengi unasaidia viungo kufanya kazi vizuri. Kunakuwa na
majimaji ya kutosha kwenye viungo yanayozuia maumivu ya viungo.
Kwa
kifupi hizo ni baadhi tu ya faida za kunywa maji ya kutosha. Kiwang cha
kunywa inabidi kisiwe chini ya glasi nane kwa siku. Kunywa maji utunze
afya yako
No comments:
Post a Comment