Mrembo
huyu ni mmoja wa watuhumiwa wa kesi hii ya wizi wa mtandao baada ya
kutumia kitambulisho chake na kutaka kuja kurudisha line ambayo sio
yake kwa kuahidiwa kupewa pesa kidogo kama ujira wake na katika melezo
yake akasema hawatambui wahusika wenzake kwani amekutana nao tu sinza na
wakampa dili hilo na kuamua kuchukua bajaji ambao iliwaleta mpaka ofisi
za tigo buguruni rozana
|
Huyu
ndio staring mwenyewe aliyechonga mchongo wote na kumshawishi huyu
mwanamke kutumia kitambuluisho chake kufanyia wizi huo wa kimtandao
|
Mrembo akijitetea kuwa hahusiki kabisa katika wizi huu na pia kujitetea kuwa kaacha mtoto mdogo nyumbani
|
Hapa akitoa maelezo kuwa yeye si mwizi na hawafahamu kabisa wahusika wenzake na yeye ni mfanyabiashara wa vipodozi
|
Watuhumiwa
wenzake wakificha sura zao huku wakitoa maelezo kwa wafanyakazi wa tigo
na walinzi waliowatia chini ya ulinzi baaada ya kuweka mtego mzuri wa
kuyanasa matapeli haya ya kimtandao
|
Hiki
ndicho kitambulisho alichokitaka kutumia huyu mwanamke kuswap line
ambayo sio yake lakini aliweka jina la mhusika wa line na namba
alizokuwa anapiga mara nyingi lakini sura yake bahati mbaya kwa umakini
wa mfanyakazi mmoja wa tigo kwa jina Octavian Rweyendera alifanikiwa
kubaini udanganyifu huo na kuamuru awekwe chini ya ulinzi mara moja
|
Aliyesimama
hapo yeye aliibiwa kiasi cha milioni moja kwa njia ya sim banking ya NMB
baada ya line kuharibika ghafla kumbe mmoja wa watuhumiwa alirudisha namba na
kuiba pesa
|
Hiki
pia ni kitambulisho cha mteja huyo hapo juu aliyeibiwa pesa kwenye
acount yake ya NMB kiasi cha milioni moja kwa njia ya NMB Mobile baada
ya mmoja wa hawa watuhumiwa kuja kurudisha laini yake kwa kutumia
kitambulisho hiki ambacho kimetengenezwa kwani si halisi na hatimaye
kufanikiwa kuiba pesa kwa sim banking baadae
|
Hapa mtuhumiiwa mmoja akiwa amejilaza chini kwa kugoma kutoa maelezo kwa walinzi waliowaweka chini ya ulinzi
|
Hapa huyu binti akilia kwa uchungu na kuomba asamehewe
|
Wakiwa ndani ya gari ya polisi kuelekea kituo cha polisi Buguruni
|
Umati wa watu uliofurika kushuhudia tukio hilo la aina yake
|
Mmoja
ya wafanyakazi mahiri wa tigo Bw Octavian Rweyendera ambaye
alifanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao akitoa maelezo kwa baadhi ya
maafande wa polisi jinsi watuhumiwa walivyotaka kufanya wizi huo wa
kimtandao
|
Askari polisi wakisikiliza kwa makini jinsi watuhumiwa hao walivyokamatwa.PICHA NA HABARI NA MWANAHARAKATI MZALENDO BLOG
|
No comments:
Post a Comment