Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, Anatory Choya akiwa amewapigia wananchi magoti kwa maana ya kuonyesha unyenyekevu
Mbulu. Mkuu
wa Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, Anatory Choya, amesema kuwa
aliwapigia magoti wananchi wa Kijiji cha Hydom, ili kuonyesha
unyenyekevu kwa wananchi hao aliodai walionekana kujazwa maneno ya
uchochezi na wanasiasa ili wavuruge amani .
Alisema
kutokana fujo zilizofanywa na baadhi ya wananchi hao katika mkutano wa
hadhara uliofanyika majuzi, kwa nafasi yake angeweza kuagiza hata Jeshi
la Polisi kuwadhibiti watu, lakini misingi ya dini yake haimruhusu
kumdhuru mtu zaidi ya kumwonyesha unyenyekevu.
Alisema hali hiyo ndiyo iliyomfanya kuamua kupiga magoti na kumshtakia Mungu.
“Mimi
ni mkristo, unyenyekevu ndiyo nguzo pekee ya kuonyesha upendo na
kudumisha amani. Ningeweza kuagiza polisi wawadhibiti, lakini sioni
sababu kwa kuwa hiyo siyo misingi ya utawala. Ndiyo maana nikaona bora
nitumie njia nyingine ya kumshirikisha Mungu mbele yao,”alisema Choya na
kuongeza:
“Wanasiasa
wamekuwa wakipandikiza chuki kwa wananchi kwa makusudi kwa lengo la
kuvuruga amani lakini kwa kumweka Mungu mbele nina imani tutafanikiwa
ili siku moja tusije tukaingia kwenye mkumbo wa Syria na Misri”
Choya
alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na Mwananchi Jumapili,
siku chache baada ya kitendo chake cha kupiga magoti mbeye ya wananchi
kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Haydom.
Mkuu
huyo wa wilaya alidaiwa pia kuwalaani baadhi ya wakazi wa Kijiji cha
Haydom kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kumdharau na kutofuata maagizo
yake, wakati yeye amewasaidia katika kutatua migogoro mbalimbali
waliyokuwa nayo.
Tukio
hilo la kusikitisha lilijitokeza baada ya wananchi wa kijiji hicho
kupinga agizo la Choya, lililowataka kufanya uchaguzi wa kaimu
mwenyekiti wa kijiji hicho, kabla ya kufanya uchaguzi mdogo, ambapo
walipinga kwa kudai kuwa hakuna sheria hiyo.
Mmoja
wa wananchi hao alilumbana na mkuu huyo wa wilaya mbapo Choya alijibu;
“Nami nitarudi kwetu." Naye Tikin akasema tena: “Unasema utarudi kwenu
Biharamulo wakati hawakutaki kwani ulifukuzwa ubunge?”
Maneno
hayo yalionyesha kumkwaza Choya ambapo alipiga magoti huku machozi
yakimlenga na kumwomba Mungu afanye jambo kwa watu wa Haydom kwani
wanamdharau kabla ya kujitokeza wazee watatu wa Haydom na kumwomba
msamaha mkuu huyo wa wilaya
No comments:
Post a Comment