Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, September 6, 2013

BARUA YA WAZI KWA MKURUGENZI MTENDAJI WA MANCHESTER UNITED - ED WOODWARD


Kwako Ed,

 Ni vigumu kujua wapi kwa kuanzia na hii barua. Sipendi kutoa maoni mabaya kuhusu klabu wala wachezaji wetu kwa kuwa naamini kila mtu anafanya kazi kwa kujituma kufanikisha mambo mzuri ambayo sie washabiki tunataka - kwa maana ya mafanikio ya uwanjani. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa takribani robo karne iliyopita chini ya Sir Alex Ferguson lakini utendaji wa klabu katika miezi kadhaa iliyopita umekuwa haueleweki.

(Kwa wale wasiokufahamu wewe, Ed) – Woodward amekuwa katika klabu tangu alipoisadia familia ya Glazer katika ununuzi wa klabu kwa £500m, alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya JP Morgan. Mwaka 2005, wakati Woodward alipojiunga na klabu - jukumu lake kubwa lilikuwa kuongeza mapato zaidi kupitia wadhamini na baishara nyingine za klabu - ukizingatia klabu inatajwa kuwa ufuasi wa mashabiki zaidi ya 660m duniani kote. Kwa hili tunaweza kusema Woodward amefanikiwa kuongeza mapato ya kibiashara ya United ambay yalikuwa kiasi cha £48million wakati alipoanza. Hivi asa mapato hayo yanafkia kiasi cha £117.6million.

Hakuna mashaka kabisa juu ya uwezo wako katika kudili na masuala ya kibiashara. Lakini kusaini mikataba ya kibiashara ya kuingiza fedha ndani ya akaunti ya Manchester United kwa hakika ni moja ya kazi rahisi kulingana na sifa na ukubwa wa klabu. Ni nani asiyetaka kuhusiana kibiashara na moja ya kampuni kubwa, maarufu zaidi duniani? Haijalishi na mafanikio ya uwanjani,  Manchester United imekuwa na itaendelea pale pale juu. Lakini mkurugenzi mkuu wa hiyo kampuni ni tofauti.
 

 Soka katika level ya juu kabisa ni kitu kigumu sana. Arsenal wamekuwa wakihangaika kupata mafanikio tangu alipoondoka  David Dein mwaka 2007, lakini kibiashara wamekuwa wakivunja rekodi kila siku. 

Klabu za soka haziwezi kuendeshwa kama ilivyo makampuni yaliyokuwa kwenye FTSE 100. Watu wa soka kama David Gill na Dein wanajua na kuelewa umuhimu wa sapoti ya mashabiki na namna inavyoweza kuathiri timu. Abramovich aliiona Chelsea ikipata taabu kwenye msimu wa 2010-11 na akaamua kucheza kamari kwa kulipa kiasi cha £50m katika kufanya usajili mmoja wa washambuliaji bora wa wakati huo Fernando Torres. Kwa bahati nzuri sisi wapinzani, uhamisho huo wa Torres haukulipa - Fernando hakuwa mchezaji yule tuliyemfahamu misimu kadhaa nyuma huko na usajili wake sasa unakwenda kwenye historia kama mmoja wa usajili mbovu wa muda wote. Lakini angalau Abramovich aliweza kufanya jaribio katika kutafuta ufanisi. Sidhani kama sisi Man United tunao ushujaa wa kujaribu namna hiyo chini yako Ed, na hilo tumelishuhudia katika harakati za kumsajili Fellaini.

Siku ambayo ilitangazwa kwamba Moyes anachukua nafasi ya Ferguson tayari ilishaonekana wazi kwamba Fellaini na Baines walikuwa wanaelekea kujiunga na boss Old Trafford. Ni miezi mitatu tangu wakati huo hivi sasa lakini ilibidi tusubiri mpaka dakika moja kabla ya dirisha la usajili kufungwa ndio tukamilishe usajili! Inabidi nikiri kwamba mfumo na taratibu nzima za namna ya kuwasajili wachezaji tunaowataka ni giza tupu kwangu, lakini kama Moyes aliamua kumsajili Fellaini mapema wakati ameingia madarakani kama kocha kwanini ilichukua muda mrefu kukamilisha usajili huo? Ilijulikana wazi kwa muda mrefu wa dirisha la usajili kwamba kuna kipengele cha kuvunja mkataba wake na Everton kwa paundi 23million. Lakini tukasubiri mpaka nyakati za mwisho mwisho za dirisha la usajili, kutokumpata mapema Fellaini kumesababisha mchezaji huyo asipate nafasi ya kujuana vizuri na wenzie, labda angekuwepo tusingefungwa na Liverpool wiki iliyopita na tumelipa £4m zaidi kwa kushindwa tu kukamilisha usajili huu mapema. Mtu mmoja inabdi abebe hizi lawama na kwa hili nadhani ni wewe Mr Woodward. Ngoja niweke wazi kwamba Fellaini ni usajili mzuri sana. Lakini tumekuwa tukihusishwa na wachezaji wengi wa daraja la juu kabisa duniani na inaonekana utendaji wako m'bovu ulifelisha suala la kuwapata wachezaji hao.

Nafasi ya beki wa kushoto ni sehemu ambayo nilihisi ilikuwa inahitaki kuimarishwa. Namkubali sana Paddy Evra. Napenda anavyjituma na anavyoonesha mapenzi kwa timu kwa kuongoza na kucheza vizuri japokuwa ni ukweli ulio wazi kwamba siku zake za kucheza soka la kiwango cha juu zinahesabika. Moyes ameliona hilo na ndio maana akawa anamhitaji Baines. Tulituma ofa ya kidharau sana huko nyuma mwezi August. Halafu ofa ya pili kwa pamoja na Fellaini ambayo ilikuwa ni ya kias cha fedha ambacho kingeweza kulipia usajili wa Fellaini. Hatukumpata mchezaji huyo wa kushoto ingawa ilionekana wazi mchezaji huyo alikuwa tayari kuhamia United. Hivyo sijui hata ikawaje kukawepo na jaribio la kumsaji kwa mkopo Fabio Coentrao na hilo pia ukazingua kwa sababu ambazo hazijawa! Hivyo sasa tumebakiwa na Evra akiwa anaingia kwenye mwaka wa mwisho wa mkataba wake tukijua klabu ijaribu na kushindwa kupata mbadala wake. Jambo ambalo halitoweza kuleta matunda nani ya klabu. 


Sakata la usajli wa Ronaldo ndio ilikuwa nafasi yako kujikaribisha binafsi na kocha mpya ndani ya uongozi wa klabu kwa staili ya namna yake. Tunafahamu kwamba kulikuwepo na mazungumzo wakati wote wa kiangazi na inaaminika Gill na Fergie wamekuwa wakihusika na suala hili tangu wakati wa mchezo wa Champions league msimu uliopita dhidi ya Madrid. Kulikuwa na nafasi kubwa ya kumnyakua mchezaji huyo kwa ada ya uhamisho labda pungufu kiasi na £80m walicholipa wao. Kumsajili Ronaldo, bila shaka kungeleta mafanikio ya uwanjani - kungeonyesha hali ya udhati wa ushindani na kuwapa mashabiki hamasa na pia kungezidi kuongeza wadhamini na kuwafurahisha wale waliopo. Pia kulikuwa na nafasi ya namna hiyo kwa Gareth Bale. Ilijulikana wazi kwamba Madrid hawakuwa na fedha za kumsajili mchezaji mpaka watakapopewa mkopo na benki hivyo kama tungekuja ofa nzuri mapema zaidi mwa dirisha la usajili tungeweza kumsajili mchezaji huyo.

Turudi kwa Fabregas. Klabu ilidhaurisha kwenye harakati za kumtaka mchezaji ambaye alionekana wazi hakutaka kuja OT na tukaishia kuwaudhi FC Barcelona na ofa zisizoisha wakati walishema kwamba hawmuuzi mchezaji huyo. Lakini kama tungechukua uamuzi mgumu na kutoa ofa nzuri zaidi ambayo ingekuwa ngumu kwao kukataa sasa hivi tungekuwa tunaongea mengine, lakini badala yake tukawa tunatoa ofa ambazo zilikuwa haziwatoi mate Barca hivyo tukaishia kupoteza muda.

Tuje kwa Ander Herrera. Inaaminika mchezaji alikuwa amevutiwa sana kuja Old Trafford  na hata alishakubali kupunguza mahitaji ya mshahara ili kukamilisha dili hilo lakini bado kwa udhaifu wako wa kudili na haya mabo uakshindwa kufanikisha usajili huu. Wewe ni kweli unastahili kwa CEO wa klabu kubwa hii Manchester United???

Moyes nadhani mpaka sasa amejitahidi kufanya kazi nzuri. Hivyo ninamuunga mkono kocha wetu mpya. Inaonekana alishagundua kwamba tuna udhaifu kwenye kiungo, beki wa kushoto. Ameweza kulishughulikia suala la Rooney, jambo limenishangaza, na sasa tumempata Fellaini tutafanya vizuri kiasi. Lakini msimu huu hautokuwa mzuri sana na hili lawama zije kwako Ed. Kama mshabiki ningependa kuangalia  timu yangu ikicheza huku kukiwa na uwepo wa Ronaldo au Fabregas kwenye kikosi chetu, lakini tunalazimika tuendelee na kina Young na Giggs. 

Naomba Sir Alex apone mapema upasuaji wake na aje kuchukua nafasi yake ndani ya bodi na kuwshughulikia wewe na wenzako. Sijawahi kushuhudia udhaifu mkubwa wa United kwenye soko la usajili kama hivi karibuni. Kufeli kuwapata wachezaji ambao kocha amewataka kunaweza kusababisha kumfelisha katika mipango yake hivyo kupelekea timu kutofanya vizuri uwanjani - na matokeo yake mpato yatashuka na wadhamini uhamia kwenye vilabu vinavyofanikiwa.


Ulikuwa na jukumu la kufanikisha kocha anapata wachezaji anaowataka. lakini umefeli. Tunaweza kumjaji Moyes kaunzia mwezi May mwakani - lakini kiukweli kabisa umetufelisha kwa kushindwa kufanikisha majukumu yako ya mwanzo tu ya kisoka na naomba usije ukarudia ujinga huu. Tunafahamu una ukaribu mkubwa na wamiliki wa timu hivyo ni vigumu kwako kutimiliwa - ila kama unaona una majukumu yaliyo nje ya uwezo wako tuachie timu yetu.
CHANZO SHAFIHDAUDA

By Manchester United Fans In Tanzania

No comments:

Post a Comment