MREMBO aliyetimuliwa shule akiwa kidato
cha nne baada ya kutundikwa mimba, Sasha Juma ameibuka na madai kuwa
amezaa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Habari kutoka kwa chanzo chetu cha
kuaminika zilidai kuwa Sasha na Diamond walikutana katika mgahawa mmoja
uliopo kwenye maduka ya Mlimani City, Dar na ndipo walipoanzisha
uhusiano.
Ilidaiwa kuwa Sasha akiwa na marafiki
zake alitoka kwenye moja ya maduka hayo ambapo alimkuta Diamond na
binamu yake, Romy Jones wakiwa wamekaa nje ya mgahawa huo.
Ilidaiwa kwamba kwa kuwa Sasha anajuana
na Romy muda mrefu, aliwafuata kisha akawasalimia ndipo Diamond
akaonekana kuvutiwa na mrembo huyo na kumwambia kuwa atachukua namba
yake ya simu ya kutoka kwa Romy kwa vile alikuwa nayo.
Chanzo chetu hicho kilizidi kutiririka
kuwa baada ya hapo Sasha aliondoka na marafiki zake, kipindi hicho akiwa
anasoma kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Dar es Salaam
International iliyopo Sinza-Kumekucha, Dar.
Ilidaiwa kuwa Diamond alianza kuchati na Sasha kabla ya kukutana na ‘kufanya yao’.
Shushushu huyo alitonya kuwa Sasha na
Diamond walikutana Sinza-Palestina, Dar wakati huo mwanamuziki huyo
alikuwa akimiliki gari aina ya Toyota Opa.
Ilidaiwa kuwa Sasha alipotimba eneo la
tukio aliingia ndani ya gari la Diamond na kuongea naye kuhusu mapenzi
ambapo msanii huyo alimwambia kitu ambacho alichovutiwa kwake ni jinsi
mrembo huo alivyofanana na Wema Isaac Sepetu ambaye aliwahi kuwa
mwandani wa jamaa huyo.
Madai yalizidi kushushwa kuwa baada ya
mwanamuziki huyo na Sasha kukubaliana walipanga kuonana kesho yake
katika hoteli moja maarufu iliyopo Sinza-Madukani, Dar ambapo msanii
huyo alimwambia mrembo huyo atangulie atapewa ufunguo na kuoneshwa
chumba na wahudumu.
Ikasemekana kwamba baadaye Diamond alifika na kuungana na wenzake chumbani.
Ilidaiwa kuwa jamaa alipotimba chumbani alimbebea ‘mtoto’ kinywaji laini aina ya Saint Anna.
‘Niuzi’ za chumbani zilidadavuliwa kuwa wakati wakiendelea kupiga kinywaji mdogomdogo ndipo staa huyo akaomba ‘mchezo’.
Ilisemekana kuwa Sasha alileta zile za
‘nataka sitaki’ lakini baadaye alimsihi kwa nguvu zote watumie kinga
ambapo mwanamuziki huyo alimwambia asijali hawezi kumpa mimba kuna mbinu
ataitumia.
Chanzo hicho kiliendelea kushusha madai
kuwa baada ya kumaliza mambo yao, Diamond alimchukulia Sasha usafiri wa
Bajaj na kumpa shilingi elfu 80 na kumwambia kuwa wataendelea
kuwasiliana.
Ilidaiwa kuwa mawasiliano yaliendelea
ambapo mwezi mmoja na nusu baadaye, Sasha alianza kujisikia vibaya na
walipopanga kukutana mara ya pili, mrembo huyo alimweleza jinsi
anavyojisikia ambapo Diamond alinunua kipimo cha kupimia mimba na kukuta
tayari Sasha alishanasa.
Ilielezwa kuwa baada ya kuona hivyo
Diamond alimsihi Sasha asitoe ujauzito huo na kumwambia kuwa akifanya
hivyo anaweza kufa na kama atajifungua yeye (Diamond) atamsomesha mrembo
huyo na kumlea mtoto wao.
Mpashaji wetu aliendelea kusema kuwa
baada ya kuachana hapo, waliendelea kuwasiliana japo siyo kama mwanzo na
baadaye mawasiliano yalikatika kabisa huku Sasha akiwa tayari
amefukuzwa shule. Mama yake Sasha alijaribu kumpigia simu Diamond lakini
msanii huyo akawa anajibu kuwa atawasiliana naye baadaye, jambo ambalo
hakuwa akilitimiza hadi alipojifungua mtoto wa kike katika Hospitali ya
Mwananyamala, Dar na kumpa jina la Rujeina.
Baada ya kupata madai hayo alitafutwa
Sasha ili kuthibitisha ambapo mwanzo alisita kuzungumza lakini baadaye
akakiri kuzalishwa na mwanamuziki huyo na kudai kuwa kwa kuwa hamjali
tena, naye aliacha kumfuatilia.
“Ni kweli nimezaa na Diamond. Mtoto ana
miezi mitatu sasa. Unajua yeye ndiye alinikatisha masomo na kusema kuwa
ataniendeleza na atamlea mtoto hivyo alivyokaa kimya sikuona tena sababu
ya kumfuatilia kwa vile kwetu napata kila kitu,” alisema Sasha.
Alipotafutwa Diamond kupitia simu ya
kiganjani akiwa Nairobi, Kenya na kupewa nafasi ya kusema ukweli juu ya
ishu hiyo, alieleza:
“Hahahaaa…mbona hiyo ishu ni kubwa sana kwangu! Ukweli huyo mwanamke simjui kabisa. Lete stori nyingine achana na hiyo.”
Katika kuonesha ‘usiriazi’, mwandishi aliendelea kumbana Diamond lakini bado alizidi kumkana Sasha.
Bado muandishi wa thesuperstarstz anazifuatilia habari hizi na tutawaletea hapa hapa majibu ya ana kwa ana kati yetu na Diamond
No comments:
Post a Comment