Pages

Tuesday, September 3, 2013

Hatimaye mnara wa kumbukumbu ya Mwangosi wajengwa,Utazame Hapa



Hatimaye ule mnara kwa ajili ya kumkumbuka mwandishi wa habari Daudi Mwangosi aliyeuwawa kwa bomu la polisi mbele ya Rpc Kamhanda wajengwa kijijini Nyololo...

Aluta continue!!
R.I.P. Mwangosi. Walaaniwe wote waliopanga, kusimamia na kutekeleza mauaji ya mtu asiyekuwa na hatia! Watu hawa ni heri wasingelizaliwa! Kamuhanda, umesimamia mauji ya Mwangosi na ukapandishwa cheo. Utadumu nacho milele? Wewe utaishi dunia hii milele? Ni furaha gani uliyo nayo moyoni kupata cheo baada ya kumwaga damu isiyokuwa na hatia. Muda si mrefu utastaafu kama ulivyosema unataka ustaafu vizuri. Hivi mtu akiua ndio anastaafu vizuri? Kifo chako hakitakuwa chema na ni wazi hata familia yako hawana amani na cheo chako kinachotokana na kuangamiza roho isiyokuwa na hatia. Ulaaniwe duniani na mbinguni!



 Mdogo wake Daudi Mwangosi akiwashukuru Chadema na wananchi wa Nyololo kwa kuweka kumbukumbu ya kaka yao mpendwa...

 via JF

No comments:

Post a Comment