HAWA NDIO MAHARAMIA 1O WANAWAKE HATARI KWA MADAWA YA KULEVYA DUNIANI
IPO
dhana kwamba wanawake ni daraja hatari sana. Machoni huonekana laini
lakini wanaweza kutenda mambo ambayo ni vigumu kwa mtu wa jinsia ya
kiume. Biashara ya madawa ya kulevya inahitaji watu hatari, katili,
wenye roho isiyotishika.
Mireya Moreno Carreon.
Nancy Botwin katika ‘siriz’ yake ya Weeds kwenye TV, anajaribu
kuonesha jinsi mwanamke anaweza kuwa hatari katika biashara ya bangi na
madawa ya kulevya kwa jumla, hata hivyo katika uhalisia, hajawafikia
hata chembe wanawake hawa hatari ambao wameitikisa dunia.
Hawa ni
maharamia 10 wauza unga, wametengeneza fedha nyingi na kila mmoja
ameshahusika kwa namna moja au nyingine na mauji. Kwa muuza madawa ya
kulevya, kitendo cha kutoa roho ya mtu kipo jirani yake sana.
1. GRISELDA BLANCO
Inawezekana huyu ndiye akawa muuza unga mwanamke katili, mwenye uwezo
mkubwa kuliko wote kuwahi kutokea katika historia ya dunia. Ameshahusika
na mauaji ya watu zaidi ya 200. Ni raia wa Colombia, akiwa na miaka 11,
tayari alishahusika na tukio la utekaji wa mtoto.
Baadaye alihamia
Marekani, kwenye Jimbo la Florida ambako alitengeneza mtandao wa madawa
ya kulevya ambao ulimpa utajiri mkubwa.
2. SANDRA AVILA BELTRAN
Ni raia wa Mexico, alizaliwa mwaka 1960. Aliwahi kupewa jina la Mungu
wa Kike wa Madawa ya Kulevya. Vyombo vya habari nchini mwake vikamwita
Malkia wa Pacific. Serikali za Marekani na Mexico zinamtaja kuwa kiungo
wa magenge ya unga ya Sinaloa Cartel la Mexico na Norte del Valle Cartel
la Colombia.
Anadaiwa kujipatia mabilioni ya dola kwa usafirishaji wa
unga kati ya Colombia, Mexico na Marekani. Kwa sasa yupo gerezani nchini
Mexico kwa kosa la utakatishaji wa fedha haramu.
3. ANGIE SANCLEMENTE VALENCIA
Ni raia wa Colombia, aliwahi kushika taji la urembo la taifa katika
nchi hiyo lakini alinyang’anywa baada ya kubaini ameshaolewa. Mume wake
alikuwa mmoja wa vinara wa unga na walipoachana, alitumia njia zilezile
kujipatia utajiri haramu.
Alikuwa na genge kubwa la wasafirishaji wa
cocaine na kila mtu alimlipa dola 5,000 kwa safari moja. Alisafirisha
zaidi Argentina, Uingereza na Mexico. Ana umri wa miaka 35, yupo
gerezani Argentina tangu Oktoba 27, 2010.
4. KATH PETTINGILL
Alizaliwa mwaka 1935. Jina lake la utani ni Bibi Kizee Shetani (Granny
Evil). Ni mwenyeji wa Jiji la Melbourne, Australia. Alianza kama kahaba
kabla ya kugeukia madawa ya kulevya.
Alipoteza jicho moja baada ya
kupigwa risasi katika moja ya matukio ya uharamia, akimtetea binti yake,
Vicky, aliyekuwa anadaiwa dola 300 na maharamia wenzake. Nguvu ya
mtandao wa unga aliyoitengeneza, ni hatari na imehusika na mauaji mengi
nchini Australia.
5. ENEDINA ARELLANO FELIX
Katika genge ambalo lilikuwa linaongozwa na kaka zake, Ramon na
Eduardo, mwanzoni yeye alishika nafasi ya umeneja wa fedha. Baada ya
Ramon kuuawa na Eduardo kukamatwa, alishika uongozi.
Maofisa usalama wa
Mexico waliwahi kukiri kwamba Enedina ndiye alikuwa dira ya kaka zake.
Ana umri wa miaka
Amebadili mfumo na sasa
anaendesha kazi zake kisayansi, hakuna fujo za magenge ya wahuni kiasi kwamba inakuwa ngumu kumtia hatiani.
6. BLANCA CAZARES SALAZAR
Ni raia wa Mexico, alianza kujihusisha na utakatishaji wa fedha haramu,
aliponogewa akajikita kwenye unga. Ana umri wa miaka 37.
Biashara yake
ameitanua na yupo makini sana. Anaongoza mtandao mkubwa wenye makundi
42. Ni ngumu kumkamata kwa sababu hahusiki moja kwa moja. Marekani
imempiga marufuku kuingia nchini humo.
7. MARIA JIMENEZ Ana umri wa miaka 27. Alikuwa
kiongozi wa genge lililokufa la La Tosca. Baada ya kufanya biashara kwa
muda mrefu, alikamatwa mwaka jana nchini kwake Mexico kwa tuhuma za
usafirishaji wa unga na mauaji. Baadaye alikiri kuua watu 20 na mpaka
sasa yupo jela.
8. EDITH LOPEZ LOPEZ
Anajulikana kama Malkia wa Kusini. Amekuwa kinara wa madawa ya kulevya
tangu alipoolewa na haramia wa unga, Raul Nunez Morales, maarufu kama
The Cowboy. Tangu mwaka 2000, Edith amebaki kuwa mmoja kati ya wanawake
tisho kwa biashara hiyo haramu duniani.
9. THELMA WRIGHT Alishirikiana na marehemu
mumewe, Jackie Wright katika biashara ya unga kati ya miaka ya 1980 na
1990. Mwaka 1986, mumewe aliuawa, kwa hiyo akashika usukani kwa kulisuka
genge lao la Black Mafia ambalo lilifanya matukio mengi.
Hata hivyo,
kwa kuhofia maisha ya mtoto wake, Jackiem, kuharibika, aliachana na
kazi hiyo na kufanya shughuli nyingine halali. Ni mara chache sana
kutokea.
10. MIREYA MORENO CARREON Ndiye
mwanamke pekee kushika nafasi ya juu kwenye Genge la Zetas. Ndani ya
kipindi kifupi alifanya matukio mengi ya utakatishaji wa fedha haramu na
usafirishaji wa unga.
Akiwa nchini kwake, Mexico, mwaka 2010, maofisa
usalama wa siri walimkamata akiwa akiwa na gari lenye cocaine na bangi
na mpaka leo yupo korokoroni.
No comments:
Post a Comment