Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, September 4, 2013

HUYU NDIO MCHEZAJI MWINGINE ALIYESAJILIWA NA MANCHESTER UNITED KATIKA SIKU YA MWISHO YA DIRISHA LA USAJILI



New kid on the block: Janko, 17, has signed for Manchester United from FC Zurich
 

Manchester United imethibitisha usajili wa kinda wa miaka 17 Saidy Janko kutoka FC Zurich.
Anajiunga na United katika dili linaloaminika linafikia kiasi cha £700,000 baada ya kuwavutia sana maskauti wa vipaji wa United katika michuano ya FIFA Blue Stars mapema mwaka huu.

Janko, ambaye alizaliwa Switzerland lakini na baba wa raia wa Gambia na mama aliyechanganya Swiss/Italian, alifanikiwa vizuri katika majaribio aliyokuwa akifanya katika kituo cha mazoezi cha United AON Training Complex kabla ya kupewa ofa ya dili la usajili. 
Janko alikamilisha usajili wake usiku wa Jumatatu akiungana na Marouane Fellaini na Guillermo Varela na kukamilisha usajili wa wachezaji wa tatu waliosajiliwa na David Moyes.
Janko hatagemewi kupewa nafasi katika kikosi cha kwanza msimu huu.

No comments:

Post a Comment