sehemu ya meza kuu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni
ya ASAS,Salim Abri akizungumza na wakazi wa mji wa Iringa na vitongoji
vyake waliojitokeza kwenye semina ya kamata fursa twenzetu,ASAS
amejitolea kiasi cha shilingi milioni tano kwa ajili ya kusaidia vikundi
vitakavyoamua kutumia fursa ya kulima vitunguu na kuendelea kuwa
wajasiliamali katika fursa mbalimbali.
Mfanyabiashara
mkubwa wa mjini Iringa,Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya ASAS,Salim
Abri akionesha baadhi ya fursa zilizopo mkoani Iringa kwa kuonesha
kitunguu cheupe kama moja ya bidhaa za thamani zinazopatikana mkoani
humo,ASAS ameeleza kuwa vitunguu hivyo vinauzwa kwa kilo kwenye
SuperMarket nyingi,anasema kuwa vitunguu hivyo vinadaiwa kutoka nje ya
nchi,lakini vitunguu hivi inawezekana kuvipanda hapa mkoani Iringa na
vijana wakanufaika kupitia mradi wa vitunguu hivyo.
Mdau
mkubwa wa michezo nchini Fredrick Mwakalebela naye alipata wasaa wa
kuzungumza na wakazi wa Iringa na kutoa kiasi cha shilingi milioni moja
kwa ajili ya kuwawezesha wakazi wa mkoa huo watakaoweza kutumia fursa ya
rasilimali zilizopo mkoani hapo.
Msanii
wa kughani mashairi Mrisho Mpoto, akizungumza na wakazi wa Iringa
waliojitokeza kusikiliza mafunzo ya namna ya kujikwamua kimaisha kwa
kutumia fursa kwa rasilimali zilizopo mjini Iringa.
Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa
Iringa wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye semina
ya Fursa kwa vijana iliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Mtakatifu
Dominic mjini Iringa,ambapo watu mbalimbali wamepata fursa ya kujua
namna ya kutumia sasilimali zilizopo mkoni humo kwa ajili ya kujikwamua
kimaisha.
Mwakilishi
kutoka NSSF Makao Makuu Salim Khalfan, akizungumzia Fursa kwa upande wa
NSSF wanavyoweza kuitumia wakazi wa Iringa katika kupata mikopo
itakayowawezesha kujikwamua kimaisha.
Mkurugenzi
wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba
akihitimisha semina ya Kamata fursa twenzetu mapema leo mchana ndani ya
mkoa wa Iringa.
Baadhi ya Wadau mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye Semina ya kamata fursa kwa vijana twenzetu.
Wanafuatilia.
Msanii
wa Muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Nick wa pili akizungumza mbele ya
sehemu ya wakazi wa Iringa ,namna ya kutumia fursa zilizopo mkoani humo
kwa ajili ya kujikwamua kimaisha.
Bwana Shamba Yona Daniel akizungumza na wakazi wa Iringa tayari kwa kuwaonyesha namna ya kutumia Fursa kupitia kilimo.
Wakifuatilia mada mbalilmbali ndani ya semina hiyo.
Meneja wa Mkoa wa Iringa kutoka
taasisi ya PSI-Tanzania,Rogers Ari akizungumza fursa mbalimbali kwa
vijana ikiwemo na suala zima la kujilinda kiafya kwa namna yoyote
ile,ili kuwa fiti katika suala zima la kuzitumia fursa wanazokumbana.
No comments:
Post a Comment