Pages

Wednesday, September 11, 2013

LISTI YA WACHEZAJI WANAOLIPWA FEDHA NYINGI SERIE A: DANIELE DE ROSSI AWAFUNIKA - HIGUAIN ASHIKA NAFASI YA PILI


Kiungo wa kimataifa wa Italy na klabu ya AS Roma Daniele De Rossi ndio mchezaji anayelipwa fedha nyingi katika ligi kuu ya Italia, hii ni kwa mujibu wa taarifa rasmi zilizotolewa na La Gazzetta dello Sport. 
Kiungo huyo mwenye miaka 30 analipwa kiasi cha 6.5 million euros kwa mwaka, akimzidi Euro millioni 1 mchezaji anayeshika nafasi ya pili Gonzalo Higuain - na millioni 2 zaidi ya nahodha wa Roma Francesco Totti.

Uchumi m'baya wa Serie unaweza kuonekana vizuri kwa namba za mishahara ya wachezaji. Ni wachezaji 12 tu katika ligi nzima ambao wamefikia au kuzidi kiwango cha mshahara wa 4 million kwa mwaka, ukilinganisha na wachezaji 13 tu wa Chelsea ambao wanairpotiwa kulipwa kiwango cha namna hiyo. 


Hakuna mchezaji yoyote kutoka kwenye ligi ya Serie A aliyeweza kuingia kwenye listi ya wachezaji wanaolipwa fedha nyingi zaidi barani ulaya, huku De Rossi akifunikwa kabisa na wachezaji wanaolipwa fedha nyingi katika vilabu vya ligi za nchi nyingine.  Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Zlatan Ibrahimovic na mshambuliaji wa Monaco Radamel Falcao wote wawili wanalipwa kiasi cha 14 million euros baada ya kodi, wakati Lionel Messi anachukua 13 million kutoka Barca, dili jipya la Gareth Bale na Madrid limemfanya mchezaji huyo kushika nafasi ya tisa miongoni mwa 10 wanaolipwa fedh nyingi zaidi.NA SHAFFIHDAUDA

No comments:

Post a Comment