Mapema Dar es salaam jana Waziri wanchi ofisi ya waziri Mkuu
sera na uratibu wa shughuli za Bunge Wiliam Lukuvi alisema Serikali inafuatilia
kwa karibu kesi zinazowahusisha Watanzania waliopo nje ya nchi wanaotuhumiwa na biashara ya dawa za
kulevya wakiwemo wanamichezo na wasanii mbalimbali.
Alisema ilikuthibitisha hali hiyo timu ya watendaji imetumwa nchini Afrika kusini hivi karibu ili
kukutana na kina Masogange kujua undani wa kesi yao na imethibitika kuhusika kweli
na tuhuma hizo ambapo inasadikiwa jana
kesi yao imesomwa rasmi na kusubiri hatua zaidi za kisheria.
Akizungumzia taarifa
za kukamatwa kwa mwanamichezo Kaniki na Matumla Lukuvi alisema taarifa hizo zitatolewa ufafanuzi zaidi na Serikali
baada ya kupokea taarifa za kiofisi kutoka nchini Ethiopia.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha kupambana na kudhibiti
na dawa za kulevya Godfrey Nzoa alisema kati ya timu waliokwenda Afrika kusini
ni pamoja na yeye mwenyewe ambaye alifanikiwa kukaa kwa karibu na wafungwa hao
akiwemo Masogange na kubaini kuna siri nzito mgongoni mwa Mwasogange hivyo
inahitaji uchunguzi ili mkono wa sheria uweze kuwagusa wote wanaohusika na
kutumia wasanii katika janga hilo.
“Ni kweli masogange na wenzie wamekamatwa na dawa aina za
Ephedrine ambazo ndio zinazotengeneza dawa za kulevya na zinaruhusiwa kuingia
nchi yeyote kwa kibali malaum kwani pia zinahusika kutengeneza dawa za kifua na timu iliyotumwa na Serikali imeweza
kuzungumza nao lakini haimaanisha kwenda kwetu gerezani tunawatetea au
tutawasaidia hapana kwakua hawakutumwa kufanya baisahara hiyo haramu ila
tunajaribu kuwa karibu ili kuona wanapata haki zao na kuweza kubaini waliopo
nyuma yao na kweli tumefanikiwa mnyororo ni
mrefu tunaendelea na uchunguzi ili kujua wafadhili na mabosi zao
tunawatiaje mikononi”alisema
Aliongeza kuwa ameshangazwa na kipato kidogo wanachopata
wasanii hao akiwemo Masogange ambapo Afande Nzoa hakutaka kukiweka hadharani
ili kupisha uchunguzi zaidi huku akiongeza kuwa kufuatia sheri iliyopo wasanii hao kesi zao
zitafanyika Afrika kusini kwakua ndiko
walikokamatiwa na endapo kuna mkataba wa ubadilishana wafungwa Serikali itaangalia
njia ya kuwasaidia ili watumikie vifungo vyao nchini.
No comments:
Post a Comment