Pages

Sunday, September 29, 2013

MATAMKO KUHUSIANA NA UJANGILI, RUAHA NATIONAL PARK

Elephant-elephants-28788754-1024-7682 2883b
MATAMKO YA WARSHA YA MANET KUHUSIANA NA UJANGILI – RUAHA NATIONAL PARK
1. Kazi ya kulinda kuhifadhi wanyamapori si jukumu la mtu mmoja wala taasisi moja bali ni ya wananchi na wadau wengine.

2. Kazi ya uelimishaji jamii kuhusiana na kulinda na kuhifadhi wanyamapori ifanyike ili jamii ishiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya ujangili.
3. Serikali isitishe utoaji kwa ajili ya uwindaji wa Tembo
4. Serikali ifanye ushawishi kwa jumuiya ya kimataifa hususan kwenye mataifa ambayo ni masoko ya meno ya Tembo
5. Sheria zilizopo za wanyamapori zirekebishwe kwa sababu hazisaidii kupunguza ujangili.
6. Serikali ifanye oparesheni ya ukaguzi wa silaha na viwanda vya kienyeji vinavyotengeneza silaha na ivifunge.
7. Serikali iharamishe utajaji wa thamani ya meno ya Tembo yanayokamatwa.
8. Serikali itoe fidia kwa uharibifu wa mazao unaofanywa na wanyamapori kwa thamani halisi badala ya kulipa kifuta jasho au kifuta machozi.
9. Serikali iongeze idadi ya wafanyakazi wa wanyamapori na vifaa vinavyohitajika hasa katika Halmashauri zinazopakana na hifadhi.

No comments:

Post a Comment