Mwenyekiti wa MANET Bw Zuberi Mwachura kulia akieleza mkakati wa kupambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha leo |
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akifafanua jambo |
Mgeni
rasmi katika warsha ya siku moja ya kujadili vitendo vya ujangili
katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha Mbunge wa jimbo la Iringa mchungaji
Peter Msigwa ( wa pili kushoto) akiwa na viongozi mbali mbali akiwemo
mwenyekiti wa taasisi iliyoandaa warsha hiyo MANET Bw Zuberi Mwachura
na viongozi wengine.
.............................. .............................. ........
Na Francis Godwin Blog, Iringa
MBUNGE wa jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha Demokrasia na
maendeleo (chadema)amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa mkakati wake
wa kunusuru vitendo vya ujangili katika hifadhi za Taifa.
Huku mbunge huyo akidai kuwa anawajua viongozi mbali mbali na watu
maarufu ambao wanaendelea kuendesha vitendo vya ujangili katika hifadhi
ya Ruaha Iringa ikiwa ni pamoja na kulitumia gari la wagonjwa
(Ambulence) kusafirisha meno ya tembo na atawataja wahusika bungeni.
Msigwa
ambae ni waziri kivuli wa wizara ya maliasili na utalii alitoa
pongezi hizo leo mjini Iringa wakati wakati akifungua kikao cha
kujadili vitendo vya ujangili katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha
Iringa iliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Mazingira
Netwark Tanzania (MANET).
"Awali
ya yote napenda kumshukuru sana Rais Jakaya Kikwete kwa kuja na
mikakati ya kweli ya kupambana na vitendo vya ujangili nchini kwa
kutumia askari wa jeshi la lawanchi Tanzania (JWTZ)...huu ni mkakati
mzuri ambao binafsi nimempongeza sana kwa hatua hiyo" alisema
Msigwa
Kuwa ni
mara kadhaa watanzania wamepata kusikia viongozi wa Serikali wenye
dhamana wakisema kuwa mtandao wa majangili na wafanyabiashara haramu wa
wanyamapori ni mpana na mgumu kuumaliza
Pia
ni mara kadhaa pia Serikali imeendelea kukiri kuwa mtandao huu
unawahusisha Wafanyabiashara wakubwa, Wanausalama, Wabunge, Wanasiasa na
watu wenye dhamana ya uongozi katika taifa letu umekuwa
ni kikwazo kikubwa katika vita dhidi ya ujangili.
“….Serikali
imeendelea kutoa matamko kuwa itawataja wahusika wa biashara haramu
dhidi ya wanyamapori na kuwachukulia hatua lakini cha kushangaza, mara
zote hakuna hatua yoyote inayochukuliwa..ni jambo moja la msingi ambalo
ningependa kulizungumza na kusisitiza hapa leo ni juu ya wajibu wa kila
Mtanzania katika kuhakikisha kuwa tunaungana kwa pamoja katika vita
dhidi ya biashara haramu ya wanyamapori”
Hivyo alisema
hatua ya Rais Kikwete kuweka mkakati huo wa kutumia askari wa
JWTZ katika kulinda hifadhi na kupambana na majangili ni jambo la
kumpongeza.
Kwani alisema
baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika tamko lake
maarufu mwaka 1961 lijulikanalo kama Arusha Manifesto alisema yafuatayo:
“Uhai
wa wanyamapori ni jambo muhimu na linalotuhusu sana sisi sote barani
Afrika. Viumbe hawa wa porini, wakiwa katika mapori wanamoishi,sio
muhimu tu kwa ajili ya kuajabiwa na kuvutia lakini pia ni sehemu
ya maliasili yetu na pia ndio mustakabali wa maisha yetu ya baadaye”.
Alisema kuwa
mwalimu Nyerere alitambua umuhimu wa kutunza wanyamapori kwa wakati huo
tukiwa na hazina kubwa ya wanyama, lakini leo viongozi wa Serikali
wameshikwa na kigugumizi katika kuhakikisha dira na jitihada za baba wa
taifa letu ,vinatimizwa.
Hivyo alisema
kama kiongozi ambaye wananchi wamenipa dhamana ya kuwawakilisha, nawiwa
kutumia nafasi hiyo, kuendeleza juhudi zangu na kuwa mstari wa mbele
katika kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anakua mdau nambari moja wa
kupinga biashara haramu ya wanyamapori kwani si tu kuwa inalitia hasara
taifa letu bali pia inaweka hatarini maisha ya wanyamapori kwa vizazi
vijavyo.
“Nachukua
nafasi hii kuikumbusha na kuitaka Serikali kutimiza wajibu wake kwa
kuwafikisha majangili na wafanyabiashara haramu wa wanyamapori katika
vyombo vya dola na watendewe ipasavyo kwa mujibu wa Sheria”
Kuhusu watu maarufu mkoani Iringa wanaojihusisha na biashara
ya pembe za ndovu na hata kutumia magari ya umma kama
Ambulence kusafirisha pembe hizo za ndovu alisema kuwa ana idadi yao
ndevu zaidi na kuwa katika kikao cha bunge kijacho ataweka hadharani
majina yao.
No comments:
Post a Comment