Waziri Prof. Mbarawa akiangalia waya wa mkongo uliokatwa
Imeandikwa na Pamela Mollel, via Jamii
blog, Arusha — Mkongo wa Taifa unakabiliwa na changamoto kubwa ya
uharibifu hata kabla haujakamilika kujengwa kwa Nchi nzima kutokana na
baadhi ya Wananchi kuhujumu Mkongo huo kwa kukata nyaya katika barabara
kuu ya Arusha - Namanga hadi Nairobi.Changamoto hiyo imeibuliwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa mara baada ya kutembelea maeneo yaliyoathirika na kuhujumiwa vibaya juzi Mkoni Arusha katika ziara yake ambapo amesema kitendo hicho kimeletea hasara Taifa. Waziri Mbarawa alisema kuwa wananchi wasio waaminifu wenye nia ya kujitajirisha hisivyo halali wamekuwa wakikata nyaya za Mkongo huo wakidhani kuwa kuna shaba ndani ya nyaya hizo.
Pia Prof. Mbarawa alisema kuwa Wakala
wa Barabara nchini,TANROADS wanawajibu wa kushirikiana na Shirika la
Simu Tanzania, TTCL kabla hawaja kabidhi mradi wa ujenzi wa Barabara kwa
Mkandarasi ili kuepuka kuharibu miundombinu hiyo yenye kuwaletea
wananchi mawasiliano, "Kilichofanywa na mkandarasi wa barabara hii siyo
sahihi kabisa wamekata nyaya na kuharibu miundombinu, kabla ya kuendelea
na shughuli za barabara walipaswa kushirikiana na TTCL," alisema
Waziri.
Watumiaji wa kubwa wa Mkongo huo wa Taifa ni pamoja na Mamlaka ya Mapato, TRA ambapo kaimu Afisa Forodha wa kituo cha Namanga, Aminiel Italisa alisema kuwa mkongo huo utarahisisha kazi zao.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Mkongo wa Taifa na mawasiliano Adin Mgendi alisema kuwa pamoja na mkongo huo kurahisisha mawasiliano hapa nchini na pia Tanzania inategemewa na nchi zilizo mbali na bahari ya Hindi ili kuziunganishwa na mkongo wa Kimataifa.
Alisema kuwa elimu inahitajika kwa wananchi ili kuelewa umuhimu wa mkongo wa Taifa jamba ambalo litapelekea mrdi huo kutohujumiwa Tanzania itatumia zaidi ya Dola za Kimarekani milioni mia mbili kukamilisha ujenzi wa mkongo huo wa mawasiliano.

No comments:
Post a Comment