Zuberi Mussa katika muonekano wa picha tofauti tofauti nje ya Ofisi ya Mtendaji Kata ya Mazinde.
Zuberi
Mussa (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mwandishi Dotto
Mwaibale (kushoto), Mashaka Kibaya (kulia) wote wa Gazeti la Jambo Leo
na Mashaka Mhando wa Gazeti la Majira mkoani Tanga, walipokwenda
kumjulia hali kijjiini kwao.
Na Dotto Mwaibale, Tanga
Zuberi
Mussa ambaye ni mpiga picha mkongwe katika vyombo mbalimbali vya habari
nchini ambaye kwa sasa anafanyakazi Kampuni ya New Habari ni mgonjwa
anayehitaji msaada wa hali na mali.
Kikubwa
kinacho msumbua mwandishi mwenzetu huyu ni ugonjwa ambao bado
haujafahamika ambapo kwa mtu anayemfahamu ni rahisi kumgundua kuwa ana
matatizo ya kiafya kwani katika kila sentesi yake ya pili na ya tatu
wakati wa kuongea naye hautaelewana naye kutokana na matamshi yake
ambayo hayafahamiki yanayoonesha kama mtu aliyechanganyikiwa.
Kutokana
na kukosekana kwa fedha za kumsaidia katika matibabu hasa Hospitalini,
Zuberi Mussa amelazimika kwenda kupata matibabu yake kwa waganga wa
jadi.
Wakati
Zuberi akiwa kijijini kwao Kata ya Mazinde wilayani Korogwe mkoani
Tanga bila ya kuwa na msaada wowote mke wa mwenzetu huyo aitwaye Rehema
Amir kwa kipindi cha mwaka mzima yupo hoi kitandani kutokana na maradhi
ya kupooza yaliyompata mwanzoni mwa mwaka jana akiwa jijini Dar es
Salaam, hawezi kufanya chochote ikiwa ni pamoja na kuongea hakika
inaumiza na kusikitisha.
Ndugu
wanahabari kila mmoja wetu kwa imani yake na utamaduni tulionao wa
kusaidiana tujitokeze kumsaidia mwenzetu huyu ambaye anapita katika
kipindi kigumu.
Binafsi
nilipofika kumuona kwa mara ya kwanza wiki iliyopita nilishitushwa na
hali aliyokuwa nayo ingawa kaka yake aitwaye Waziri Mussa anayemuuguza
alidai kuwa alikuwa amepata nafuu.
Zuberi
alifika katika eneo nililokuwepo akiwa katika hali ambayo si ya kawaida
zaidi ya kusalimiana na kunitambua mengine yote nilioongea naye
hatukuweza kuelewana. Kwa mtu yeyote atakayependa kumsaidia Zuberi
pamoja na mke wake kipenzi Rehema Amir anaweza kuwasiliana na Dotto
Mwaibale kwa namba 0712-727062 ambaye atakuunganisha na kaka yake.
Ndugu
wanahabari wenzangu na mtu mmoja mmoja, Taasisi yoyote, shirika lolote,
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Wafanyabiashara, Makampuni mbalimbali
na vyama vya michezo hima tujitoe kimasomaso kumsaidia mpiga naji
mwenzetu Zuberi Mussa na mke wake waondoke katika matibabu ya jadi
wanayopata kwa waganga wa kienyeji badala yake wapelekwe hospitali kwa
uchunguzi zaidi wa afya zao kwani kutoa ni moyo na si utajiri.
duh!+nampa pole sana
ReplyDeleteamwamini na kumtegeme Mungu pekee
ndiye atakae mponya