Ngassa katika gari lake jipya |
Sasa
Ngassa anakuwa na gari 10, kati ya hizo kuna mbili alizowapa wazazi
wake, baba na mama yake moja ya familia na tatu za kibiashara.
Kwa
sasa, Ngassa ameuwambia mtandao wa BIN ZUBEIRY atakuwa anatumia zaidi
‘mkoko’ wake mpya badala ya ile Nissan ambayo amekuwa akionekana nayo
siku za karibuni.
Wakati
fulani, alionekana na Prado kwenye mazoezi ya Yanga na kuhusu gari
hilo, Ngassa anasema; “Halikuwa gari langu lile, kuna mjomba wangu
alichukua gari langu akaniachia lile la kwake,”alisema.
Kwa sasa Ngassa yuko Mwanza alipokwenda kuhudhuria mazishi ya bibi yake mzaa baba, Bi Joha aliyefariki dunia mapema wiki hii.
Magari ya Ngassa yamepagana nyumbani kwake |
Ni gari kali |
Mtoto
huyo wa kiungo wa zamani wa Simba SC, Khalfan Ngassa ‘Babu’ anatarajiwa
kupanda ndege leo mjini Mwanza kwenda Mbeya kuungana na timu yake,
Yanga SC ambayo ipo huko kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya
wenyeji Mbeya City kesho.
Hata
hivyo, Ngassa kwa sasa hachezi kutokana na kuwa bado anatumikia adhabu
ya kufungiwa mechi sita na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) kwa kusaini timu mbili, Simba na Yanga SC. Tayari amekosa
mechi tatu.
No comments:
Post a Comment