Msanii Dully Sykes ametangaza kuwa
anauza studio yake ya Dhahabu Rec iliyoko Tabata kwasababu anataka
kubaki na studio moja ambayo ni 4.12.Dully alisema kuwa kwa yeyote
ambaye atajitokeza kununua studio hiyo atamuuzia vifaa vilivyopo
ndani pamoja na jina la Dhahabu Rec.Kwa yeyote anayetaka kununua
studio hiyo amtafute.
Wakati huo huo msanii huyo ambaye yupo
kwenye orodha ya wasanii wenye nyimbo 'hits' nyingi hapa
Tanzania,kwa mujibu wake mwenyewe 56,alisema kuwa
tangu aanze muziki mpaka leo hajawahi kutumia hela yake ya mfukoni
kulipia wimbo wowote studio.Dully pia anasema anatarajia kuachia
wimbo wake mpya wiki ijayo unaoenda kwa jina la 'Kabinti Special'
wimbo ambao anasema ameufanya kwaajili ya mashabiki wake wa
kike,”video iko tayari,siku itakapofika ntaachia wimbo na video
hiyo ambayo anaamini ina ubora wa hali ya juu”, Dully.CHANZO ANNA PETER
No comments:
Post a Comment