Mwanamke wa Kitanzania kwa jina Gaga Moza (25) amefariki dunia nchini India baada ya ku-overdose dawa za kulevya. Kwa mujibu wa polisi wa India, Moza na rafiki yake wa kiume walikwenda kwenye party moja ambayo ilihudhuriwa na Wanaigeria wengi iliyofanyika kwenye basement ya hoteli ya Stallion, iliyoko eneo linalojulikana kama Safdarjung Enclave karibu na soko la Green Park kusini mwa Delhi.
Kwa mujibu wa polisi, Gaga alikuwa anaishi na rafiki yake wa Kiafrika katika eneo lijulikanano kama South Extension II. Polisi wanadai Gaga alianguka kwenye party hiyo baada ya ku-overdose dawa za kulevya. Siku iliyofuata, roomate wake aliyejulikana kwa jina Sabina alimpeleka Gaga katika hosipitali ya Sukhmani lakini madaktari walikuta tayari alikuwa ameshafariki.
Polisi wamesema kuwa kwa mujibu wa ripoti za kitibabu na maelezo kutoka kwa mashuhuda, marehemu alifariki baada ya kutumia dawa za kulevya, kama cocaine, huku akichanganya na pombe.
Polisi wamefunga basement ya hoteli hiyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Pia polisi wamemkamata meneja wa hoteli, msaidizi wake na pia rafiki wa kiume wa marehemu kwa mahojiano zaidi. Aidha polisi wanaendelea kumtafuta mtu ayeandaa hiyo party.
Kwa mujibu wa polisi, kinachosubiriwa sasa ni ripoti ya postmortem na tayari wameshafanya mawasiliano na ubalozi wa Tanzania ili kuwataarifu ndugu na jamaa kuhusiana na kifo hicho.CHANZO JF
MWENYEKITI COREFA AJIFUNGA MKANDA KUFUFUA SOKA LA UFUKWENI PWANI
-
NA VICTOR MASANGU,PWANI
Chama cha soko Mkoa wa Pwani (COREFA) katika kuunga mkono juhudi za Rais wa
awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kukuza se...
11 hours ago
No comments:
Post a Comment