Pages

Wednesday, September 4, 2013

MWENGE WA UHURU WATUA NA KUKABIDHIWA RASMI MKOA WA DAR ES SALAAM LEO



 Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sauda Salum Mtondoo(kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania  Hajati Mwantum Mahiza (kushoto) kwa ajili ya kuukabidhi Mwenge kwa Mkoa wa Dar es Salaam, katika makabidhiano yaliyofanyika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mmoja wa wakimbiza Mwenge Kitaifa Zamda John (Tanga) katika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Juma Ali Simai akitoa salamu za shukrani kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Hajati Mwantum Mahiza (aliyevaa Miwani) kabla ya kuukabithi Mwenge huo kwa Mkoa wa Dar es Salaam, katika makabidhiano yaliyofanyika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.
Picture 402 -Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Said Meck Sadiki akitoa taarifa fupi mara baada ya kupokea Mwege wa Uhuru leo Jijini D
 Kaimu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo(kushoto) akipokea Mwenge wa uhuru kutoka kwa Mmoja wa wakimbiza mwenge kitaifa, katika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Said Meck Sadiki (kulia) akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania  Hajati Mwantum Mahiza (kushoto) katika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Said Meck Sadiki akitoa taarifa fupi mara baada ya kupokea Mwege wa Uhuru leo Jijini Dar es Salaam katika uwanja wa ndege wa Terminal one.
 Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Barnabas Ndunguru akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mmoja wa wakimbiza mwenge kitaifa kabla ya Mwenge huo kukabidhiwa kwa Mkoa wa Dar es Salaam Kulia ni Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Assah Mwambene.  Picha na Hassan Silayo-MAELEZO

No comments:

Post a Comment