Pages

Thursday, September 19, 2013

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo azindua Rocky City Marathon



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel akikata utepe kuashiria uzinduzi wa awamu ya tano ya Mbio za Rock City Marathon 2013, leo Jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Capital Plus International (CPI), Dkt. Hellen Otaru Okoedion. Mbio hizo zinazoandaliwa na kuratibiwa na CIP zinatarajiwa kufanyika  mkoani Mwanza tarehe 27 Oktoba, mwaka huu.


Katibu Mkuu wa Chama cha Wanariadha Tanzania, Bw. Suleiman Nyambui (katikati) akimueleza jambo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel baada ya uzinduzi wa awamu ya tano ya mbio za Rock City Marathon leo Jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Precision Air, Bibi Linda Chiza ambao ni mmoja wa wadhamini wa mbio hizo.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati aliyevaa suti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na waandaaji, wadhamini na watendaji wa Baraza la Michezo Tanzania wakati wa uzinduzi wa awamu ya tano ya mbio za Rock City Marathon leo Jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bw. Dioniz Malinzi, wa pili ni Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Capital Plus International, Dkt. Hellen Otaru Okoedion na wa kwanza kushoto ni Katibu Mtendaji wa BMT, Bw. Henry Lihaya. Mbio hizo zinazoandaliwa na kampuni ya Capital Plus International zinatarajiwa kufanyika mkoani Mwanza tarehe 27 Oktoba, mwaka huu.
(Picha zote na Concilia Niyibitanga

No comments:

Post a Comment