PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.
…………………..
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mhe. January
Makamba amezindua rasmi mkutano wa Washikadua juu ya uanzishwaji wa Tume
ya TEHAMA leo jijini Dar es Salaam.
Mhe.
Makamba amesema kuwa TEHAMA kitakuwa chombo kikubwa ambacho
kitashirikisha wadau wengi hapa nchini kwa lengo la kuhakikisha kuwa
matumizi ya TEHAMA yanasonga mbele na inatoa fursa mbalimbali zenye
kuweza kutatua changamoto za kimaisha kwa watanzania.
Mhe.
Makamba aliongeza kuwa TEHAMA ndiyo inaleta mabadiliko na kuleta
maendeleo makubwa hivyo amesisitiza juu matumizi ya TEHAMA katika ofisi
za serikali na sekta binafsi. Aidha, amewashauri wadau wote kuangalia
wenzetu nchi zilizoendelea jinsi wafanyavyo ili kuhakikisha kuwa
matumizi ya TEHAMA nchini Tanzania yanasonga mbele.
“Kama
Taifa hakuna sehemu ambapo tunakutana kutafakari juu hali ilivyo katika
matumizi ya TEHAMA hapa nchini”. Alisema Mhe. Makamba.
Kwa
upande mwingine Mhe. Makamba alisisitiza juu ya wanataaluma wa TEHAMA
wawe wanajulikana na amesema kuwa katika uundaji wa Tume hiyo ni vema
wataalamu na ufanisi wa kazi zao ujulikane ili kuepukana na kuwa na
wataalamu ambao ni Makanjanja.
“Hapa
nchini Tanzania hatuna uhakika wa wahitimu katika mambo ya TEHAMA hivyo
kuna uwepo wa vyuo na tasisi ndogondogo nyingi zilizosambaa ambazo
zinajikita kutoa taaluma hiyo, katika masuala ya TEHAMA ni lazima
wataalamu wajulikane na kusajiliwa kama ilivyo katika bodi nyingine za
serikali hapa nchini”. Alisema Naibu Waziri.
Aidha,
Mhe. Makamba alimalizia kwa kuipongeza Serikali kwa kazi kubwa
inayofanya kwa upande wa TEHAMA kwani mpaka hivi sasa nchi imefikia
mahali pazuri katika mambo ya mawasiliano pia ameshauri juu ya
ushirikishwaji wa sekta binafsi katika uundaji wa tume ya TEHAMA.
No comments:
Post a Comment