Hali
ya wasiwasi imezidi kutanda kwa baadhi ya watu kisiwani Zanzibar
baada ya Padri Anselmo Mwangamba(pichani) wa Parokia ya Mpendae
kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana leo majira saa 10 jioni .Padri
Mwangamba ambaye ni Mkuu wa kituo cha malezi cha vijana kilichopo Cheju
Mkoa wa Kusini Unguja ambacho hutunza vijana kwa ajili ya kuwapatia
mafunzo mbali mbali alikumbana na mkasa huo wakati akitoka kupata huduma za mawasiliano ya mtandao katika maeneo la Mlandege.
Taarifa
toka kwa Daktari wa hospitali ya Mnazi mmoja ambaye alimpokea padri
huyo Dr. Abdalla Haidari alisema Padre huyo ameumia sehemu ya uso na
kifua, inaonyesha amejeruhiwa na maji ambayo baada ya kuyafanyia
uchunguzi tumegunduwa kuwa ni tindikali . Pia mfanyakazi mmoja wa duka
linalotoa huduma za mawasiliano ya mtandao aliyejitambulisha kwa jina la
Salma (kwenye video) alikiri kutokea kwa tukio hilo na kukiri kuwa
huyo padre ni mteja wake na alipata huduma hapo dukani kwake.
Hilo ni tukio la tano kwa watu mbali mbali kumwagiwa tindikali huko Zanzibar, tukio
hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa mjini Magharibi
Unguja, Mkadam Khamis na amedai uchunguzi wa kina umeanza.

No comments:
Post a Comment